MAJALIWA AFUNGUA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA MJI MBINGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 4, 2021 amezindua jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Mkoani Ruvuma.

Pia, Waziri Mkuu alikagua nyumba 7 za Wakuu wa Idara za  Halmashauri ya Mji wa Mbinga zilizojengwa  na Serikali kwa gharama ya sh. Milioni 321.771.

Nyumba za Wakuu wa Idara  za Halmashauri ya wilaya ya Mbinga  ambazo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizikagua Januari 4,2020.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme wakifungua Jengo la Ofisi  za Halmashauri ya Mji  Mbinga, Januari 4, 2021.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Grace Quintine amesema lengo la miradi hii ni kuboresha mazingira ya makazi ya watumishi wa halmashauri ikiwa ni pamoja na kupunguza kilipa posho za nyumba kwa kila mwezi

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Ruvuma, Hamza Mwenda ahakikishe anawakamata viongozi wa AMCOS kwa tuhuma za kutoa fedha za wanachama na kuwapa madiwani ili wakawashawishi madiwani wenzao wakubali kubadilisha eneo la ujenzi wa ofosi za Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua jengo la Utawala la Halmashauri ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma, Januari 4, 2021.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.