Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akipata taarifa kuhusu kampuni ya TEHAMA ya Magila Tech iliyoanzishwa na Godfrey Magila (anayezungumza) wakati wa ziara yake kwenye Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA KUENDELEZA VIJANA WABUNIFU WA TEHAMA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akipata taarifa kuhusu kampuni ya TEHAMA ya Magila Tech iliyoanzishwa na Godfrey Magila (anayezungumza) wakati wa ziara yake kwenye Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali itaweka mazingira wezeshi ya kuendeleza vijana wabunifu wa TEHAMA nchini

Ndkt. Ndugulile ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (COICT) zilizopo Dar es Salaam

Ad
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia) akimsikiliza Anorld Matemu (anayezungumza), mbunifu wa mfumo wa TEHAMA wa kupima ubora wa maji wakati wa ziara yake kwenye Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam

Amesema kuwa vijana wanabuni mifumo mbali mbali ya TEHAMA ya kutatua changamoto za wananchi ila wanakosa mazingira wezeshi ya kuendeleza na kukuza bunifu zao kama vile kupatiwa muda maalumu wa kuingiza sokoni bunifu zao kwa kufanya majaribio ya bunifu hizo kukubalika kwa wananchi bila kulazimika kulipia gharama za usajili, kupata masoko, malipo ya kodi na leseni kuendana na matakwa ya uendeshaji wa kampuni na biashara nchini

Amesisitiza kuwa azma ya Serikali ni kuendeleza wabunifu wa TEHAMA ili waweze kutengeneza mifumo kuendana na mahitaji ya wananchi badala ya kuendelea kununua mifumo hiyo kwa gharama kubwa kutoka nje ya nchi ambapo Serikali inatumia fedha nyingi kununua mifumo ya TEHAMA

Mkuu wa Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Mussa Kisaka akitoa maelezo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kushoto) kuhusu kampuni za TEHAMA zinazobuniwa na wanafunzi wa Chuo hicho wakati wa ziara yake chuoni hapo, Dar es Salaam

Amefafanua kuwa utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA hapa nchini utaongeza wigo wa matumizi ya intaneti na huduma za mawasiliano na itajibu changamoto za wananchi na ametoa rai kwa watanzania kujenga imani ya kutumia teknolojia rahisi zinazobuniwa na vijana wa ndani ya nchi bila kujali umri, uzoefu au majina ya kampuni zao

Naye Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu amesema kuwa vijana haom wameanzisha kampuni zaidi ya 20 za mifumo ya TEHAMA na tayari mifumo hiyo inasaidia kukusanya kodi kwenye halmashauri; kuwawezesha vijana kusoma VETA kwa njia ya mtandao na TIGO kuweza kuhifadhi taarifa za wateja wake

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akimsikiliza mwalimu wa vijana wabunifu wa TEHAMA, Dickson Kamala wakati wa ziara yake kwenye Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu, utafiti na ubunifu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Benadetha Kiliani na Mkuu wa Ndaki ya TEHAMA ya Chuo hicho, Dkt. Mussa Kisaka wamesema kuwa Chuo kiko tayari kushirikiana na Wizara ili kuendeleza vijana wabunifu na watafiti wa TEHAMA nchini

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Alvina Minja kuhusu mfumo wa TEHAMA alioutengeneza wa kuwawezesha wazazi kupata taarifa za wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wakati wa ziara yake kwenye Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar Salaam, Dar es Salaam

Akizungumza kwa niaba ya vijana wabunifu wa TEHAMA, Geofrey Magila ameiomba Serikali kuwawezesha wakubalike na kuaminika na wapewe kazi badala ya kampuni zao kufanya kazi kwa kutumia mgongo na majina ya kampuni nyingine kwa kuwa kampuni zao ni changa na hazina mtaji wa kutosha kuingia kwenye ushindani wa zabuni zinazotangazwa zinazohusu mifumo ya TEHAMA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) akimsikiliza Saida Ally, mkufunzi wa TEHAMA kwa wasichana alipotembelea Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam

“Tulipata kazi kutoka kampuni ya AIS ya simu za mkononi ya Malyasia yenye wateja zaidi ya milioni 50 ambao walituamini na tuliwatengenezea mifumo ya kulinda taarifa za wateja wao, ndipo baadae baadhi ya kampuni za ndani ya nchi zikaanza kutuamini,” amesema Magila

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *