WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA SAFARI ZA MV MBEYA II

Muonekano wa ndani wa Meli ya MV. Mbeya II ambayo imezinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 5, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Muonekano wa ndani wa Meli ya MV. Mbeya II ambayo imezinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 5, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Januari 5, 2020) amezindua rasmi safari ya meli mpya ya MV Mbeya II katika Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa itakayotoa huduma katika Ziwa Nyasa nchini na nchi jirani za Msumbuji na Malawi.
 
Meli hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 9.1 ni muendelezo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria kwa lengo la kuboresha uchumi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe  kupiga king’ora kuashiria uzinduzi wa Meli ya MV. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitumia kionambali wakati alipozindua Meli ya Mv. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. Wa pili kushoto ni Mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme
. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Meli ya MV. Mbeya II kwenye Bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa, Januari 5, 2021. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,Deusdedit Kakoko, Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya,Mwenyekiti wa Bodi ya MNamlaka ya Bandari Tanzania, Ignas Rubaratuka na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka  kwenye Meli ya MV Mbeya II baada ya kuizindua kwenye Bandari ya Mbamba Bay Januari 5, 2021.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Mkuu amewataka wananchi waitunze meli hiyo

Ad

Aidha, Waziri Mkuu amesema Tanzania imezungukwa na nchi nane ambazo zinategemea kupata bidhaa mbalimbali kutoka nchini hivyo Wananchi watumie fursa ya uwepo wa meli hii kufanya biashara.
 
Amesema wananchi hawawezi kupata maendeleo bila ya Serikali kujenga miundombinu kama ya meli, barabara, bandari, hivyo amewataka waitumie vizuri kwa ajili ya kukuza uchumi wao.
 
Meli hiyo imejengwa na kampuni ya Kitanzania ya Songoro Marine

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA RAIS WA JAMHURI YA KENYA DKT. WILLIAM SAMOEI RUTO, NAIROBI NCHINI KENYA

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.