DKT. NDUGULILE ATAKA TEKNOLOJIA RAHISI ZITUMIKE KUFIKISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akiwaonesha na kuwataka Menejimenti na wafanyakazi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote watekeleze Ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 na hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati akifungua Bunge wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo, Dodoma. Katikati ni Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Justina Mashiba

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amesema anataka kuona Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mpya inayoendana na Wizara mpya wakati wa ziara yake alipotembelea taasisi hiyo iliyo chini ya Wizara yake na kufanya kikao na wajumbe wa bodi, menejimenti na wafanyakazi ili kufahamiana na kuwa na uelewa wa pamoja kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa makujumu ya Wizara hiyo mpya ili kuakisia maono na ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuunda Wizara hiyo mwezi Desemba, 2020

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akimshukuru Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba (wa kwanza kulia) baada ya kupokea vitabu vya taasisi hiyo vyenye taarifa ya ujenzi wa minara ya mawasiliano nchi nzima wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo, Dodoma. Katikati aliyeshika vitabu hivyo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula

Dkt. Ndugulile amesema kuwa hivi sasa UCSAF inatumia shilingi milioni 350 kujenga mnara mmoja wa mawasiliano kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara, mbuga za wanyama, misitu na mipakani ambapo amesema gharama hiyo ni kubwa hivyo ameitaka UCSAF kubuni teknolojia rahisi zitakazotumika kuongeza wigo wa kufikisha huduma za mawasiliano nchini kwa gharama nafuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo, Dodoma. Wa kwanza kulia anayesikiliza ni Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Justina Mashiba

Pia, ameongeza kuwa Wizara ishirikiane na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kufanya utafiti ili kubaini mchango wa TEHAMA katika ukuaji wa uchumi kwa kuwa taarifa iliyopo sasa ni kuwa TEHAMA inachangia pato la taifa kwa asilimia 0.5 wakati taasisi za Serikali, sekta binafsi na wananchi TEHAMA na huduma za mawasiliano kwa kiasi kikubwa

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Godfrey Simbeye akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kushoto) wakati wa kikao cha Waziri huyo na wajumbe wa bodi hiyo, Dodoma.

Amesema kuwa Wizara ikamilishe uandaaji wa sheria ya TEHAMA na kuboresha sheria zilizopo za taasisi za Wizara hiyo pamoja na kanuni ili ziweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani ili TEHAMA iweze kufanikisha zaidi ukusanyaji wa mapato na kuwekeza zaidi kwenye TEHAMA kwa kuwa ukiongeza asilimia 1% ya uwekezaji kwenye TEHAMA inachangia pato la taifa kwa asilimia 10%

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula (wa pili kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote baada ya kikao chake na wajumbe hao, Dodoma
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa menejimenti ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote baada ya kikao chake na wajumbe hao, Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Justina Mashiba

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema kuwa wameambatana na Dkt. Ndugulile kwenye ziara hiyo ili kutengeneza dira ya pamoja ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kidijitali. Naye Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba amesema kuwa hadi sasa wamefikisha huduma za mawasiliano kwenye vijiji 3,119 vilivyopo kwenye kata 994 zenye wakazi 12,241,492 na amekiri kufanyia kazi maelekezo ya Waziri huyo ili wananchi wengi zaidi wapate huduma za mawasiliano

Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Anastasius Pessa (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza (katikati) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Kitolina Kippa (wa kwanza kulia) wa Wizara hiyo wakimsikiliza Waziri wao, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na menejimenti na wafanyakazi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Dodoma

Na Prisca Ulomi, WMTH

Naye Afisa Mhasibu Mkuu wa UCSAF, Josephine Mtei amesema kuwa ziara ya Waziri huyo na viongozi wa Wizara ni jicho la taasisi yao la kuona utendaji wao na wako tayari kushirikiana na Wizara kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi wengi zaidi ili kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2020- 2025

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.