Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 – 12 Januari 2021 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Akithibitisha juu ya ziara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa Mhe. Nyusi atawasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa ndege wa Geita – Chato
