RC ARUSHA APONGEZA KAMPENI YA UJENZI WA MADARASA ARUMERU

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta amempongeza mkuu wa wilaya ya Arumeru na uongozi mzima wa halmashauri ya Meru, na Halmashauri ya Arusha Dc kwa hatua nzuri waliyofikia katika ujenzi wa madarasa.

Kimanta ambae amefanya ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa katika halmashauri za Meru na Arusha amesema kasi ya ujenzi inaridhisha na kuwataka kuendelea na kamapani ya ujenzi endelevu wa madarasa katika wilaya ya Arumeru kampeni inayoratibiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Halmashauri za meru na Arusha Dc pamoja na wenyeviti wa Halmashauri zote mbili na wabunge wa Arumeru mashariki na Arumeru Magharibi

Muonekano wa madarasa ya shule

Mkuu wa Mkoa Kimanta pia amefurahishwa na jitihada za ujenzi wa shule tatu mpya za Faye Crane chemchem ambayo ni ya primary na Shule ya sekondari ya elimu maalum Patandi zote zikiwa za serikali Halmashauri ya meru pamoja na shule ya mchepuo ya Kingereza ya Mringa ambayo inamilikiwa na Halmashauri ya Arusha Dc shule zote ziko katika hatua za mwisho za kukamilika na zitaanza kupokea wanafunzi mwaka huu 2021

Akitoa taarifa kwa Rc Kimanta, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amesema Mpaka kufikia tarehe 18.01.2021 madarasa jumla ya 30 yatakuwa yamekamilika na kabla ya tarehe 28.02.2021 madarasa 28 yatakuwa yamekamilika na kufikia idadi ya madarasa 58 yanayoitajika kwa msimu huu kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro anayezungumza
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.