WAZIRI ELIMU NDALICHAKO AKAGUA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA

Muonekano wa baadhi ya majengo yanayojengwa katika Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Mkoani Kagera

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekagua mradi wa ujenzi wa Chuo kipya cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) katika  Mkoa wa Kagera.

Profesa Ndalichako amefanya ukaguzi huo Januari 9, 2021 wakati wa ziara ya siku moja mkoani humo ambapo amesema ameridhishwa na utekelezaji wa  Mradi huo ambao umefikia asilimia 50.7 ili kukamilika na ubora wa majengo yanayojengwa katika eneo hilo.

Ad
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigadia General Marco Gaguti na Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu wakikagua uimara wa moja ya jengo lililojengwa katika Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera wakati wa ziara mkoani humo.

Waziri Ndalichako amemtaka mkandarasi Shanxi Construction Investment Group Company Limited. kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema ili ifikapo mwezi wa nane mwaka huu uwe umekamilika.

“Kukamilika kwa mradi huu kutafanya Serikali iendelee kutimiza azma ya kuhakikisha inatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wengi zaidi wa Kitanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa viwanda.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigadia General Marco Gaguti wakisikiliza maelezo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera kutoka kwa Mhandisi Frank Ngao

Naye Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi  nchini, Dkt. Pancras Bujulu amemweleza Waziri Ndalichako kuwa utekelezaji wa ujenzi wa majengo umefikia asilimia 50.7 na kwamba majengo yote yamekamilika  yakisubiri kazi ya uezekaji paa huku kazi ya kusawazisha ardhi na mazingira ikiendelea.

Dkt. Bujulu amesema ujenzi wa wa chuo hicho unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Watu China kwa gharama ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 22.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *