NAIBU WAZIRI KASEKENYA AWATAKA WATENDAJI KUFANYA MAAMUZI

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (aliyevaa suti ya kaki) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Uchukuzi, lililofanyika kwa siku mbili mkoani Mwanza

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameitaka menejimenti na viongozi wa taasisi wa Sekta ya Uchukuzi kufanya maamuzi ili kutochelewesha maendeleo kwa wananchi katika utekelezaji wa miradi.

Ametoa kauli hiyo wakati akifunga Mkutano wa siku mbili wa baraza la Wafanyakazi la sekta ya Uchukuzi lililofanyika Mkoani Mwanza na kusema kuwa awamu hii imejikita katika matokeo na sio mazoea.

Ad

“Katika awamu hii watendaji wengi wamekuwa wakichelewa kutoa maamuzi katika maeneo mbalimbali sababu ya kutojiamini hii inafanya utekelezaji wa miradi kuchelewa kukamilika na kuchelewesha maendeleo kwa wananchi” amesema Mhandisi Kasekenya.

Mhandisi Kasekenya ametabaisha umuhimu wa kuwa na ratiba ya ukaguzi wa miradi kwa kila muhula na kusisitiza kuwa ukaguzi huo utawezesha kupunguza changamoto zinazojitokeza kwenye utekelezaji wa miradi.

“Namna bora ya kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye miradi ni kuwa na ratiba ya kukagua miradi hiyo mara kwa mara, na ratiba hizo zipangwe kwa miradi yote inayotekelezwa chini ya Sekta’ Amesisitiza Mhandisi Kasekenya.

Aidha, Mhandisi Kasekenya amesema kuwa ni muhimu wataalam wa sekta walio kwenye miradi kuchukua ujuzi wakati huu ambapo miradi inaendelea ili utaalam huo uwasaidie kusiimamia vizuri miradi itakapokamilika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza na Kaimu Katibu Mkuu Gabriel Migire ameahidi kutekeleza maagizo hayo na kusisitiza kuwa kitengo cha Ufatiliaji na Tathimini-Uchukuzi kitaboresha zoezi hilo na kuhakikisha linafanyika na kuleta matokeo chanya.

Baraza la Wafanyakazi la sekta ya uchukuzi lililofanyika kwa siku mbili mkoani Mwanza limejumuisha menejementi na watumishi wa kila idara katika sekta na wakuu wa taasisi zilizo chini yake ambapo pamoja na mambo mengine limepitia utekelezaji wa miradi ya sekta na kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji wa sekta.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *