NAIBU WAZIRI SILINDE AIPONGEZA WILAYA YA ARUMERU KWA UJENZI WA MADARASA

Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe David Silinde (Mb) ameipongeza wilaya ya Arumeru pamoja na Halmashauri zake mbili za Meru Dc na Arusha Dc kwa kazi ya ujenzi wa madarasa pamoja na usimamizi madhubuti wa fedha za Umma za miradi ya EP4R

Mhe Silinde ambae amefanya ziara leo Tarehe 14/01/2021 katika wilaya ya Arumeru ameonyeshwa kuridhishwa kwa kiwango kikubwa cha namna Halmashauri za Meru Dc na Arusha Dc zilivyoweza kutekeleza kwa vitendo maagizo ya Mhe Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Majaliwa ya ujenzi wa madarasa ambayo kwa Wilaya ya Arumeru madarasa yote yanayojengwa ni ya kisasa kwa gharama nafuu

Katika hatua ingine Mhe Silinde ameonyesha kufurahishwa na maamuzi ya ujenzi wa madarasa kwa mtindo wa magorofa unaofanywa na Halmashauri ya Arusha Na Meru hatua inayosaidia kuondokana na changamoto ya uhaba wa Ardhi

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.