HOSPITALI YA UHURU YAANZA KUTOA HUDUMA

Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akizungumza jambo na manesi wanaofanya kazi katika hospital ya uhuru iliyopo Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.Hospitali hiyo ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.8, imeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.

Hospitali ya Uhuru inayojengwa kwa gharama za bilioni 3.9 imeanza  kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt. Dkt.Eusebius Kessy alipokuwa akiongea  na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo

Ad

“Hospitali yetu imeanza kutoa huduma tangia tarehe 21 Desemba 2020 na mpaka sasa imeshahudumia wateja takribani 300”amesema Dkt Kessy

Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akikagua vifaa mbalimbali vilivyopo katika hospitali ya Uhuru ambayo imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.

Ameongeza kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa chamwino na maeneo ya karibu na kusema kuwa watahahakisha kwamba huduma zinakuwa bora kama ilivyokusudiwa

Dkt kessy amesema kuwa hospitali iyo inatoa huduma kwa wagonjwa wenye bima ya afya ya Taifa NHIF na Mfuko wa afya ya jamii (CHF) na pia wale ambao hawana bima ya afya.

Akizungumzia huduma zinazotolewa kwa sasa Dkt.Kessy amesema kwa sasa huduma za maabara,clinic za macho na meno,mionzi ,clinic za mama na mtoto na huduma za wagonjwa wa nje (OPD).

Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akipata maelezo kutoka kwa Mganga mkuu wa halmshauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt.Eusebius Kessy (kulia) juu ya mashine mbalimbali zilizoletwa hospitali ya uhuru iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma

Kwa upande wake Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe ambae alifanya ziara maalum kukagua imaendeleo ya Hospitali hiyo amesema kuwa kuwa ujenzi wa hospitali iyo umekamilika kwa asilimia 99.8.

Amebainisha kuwa maagizo yaliyotolewa na Waziri mkuu alipofanya ziara Novemba 20,2020 yametekelezwa ikiwemo kukamilisha ujenzi wa jengo ifikapo tarehe 5 Desemba 2020,vigae vya chini,miundombinu muhimu na ukamilishaji wa ukuta kuzunguka hospitali hiyo ambao umekamilika kwa asilimia 99 na ujenzi wa miundombinu ya barabara hospitalini hapo unaendelea chini ya TARURA na utakamilika hivi karibuni.

Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akipata maelezo mbalimbali juu ya huduma zinazotolewa katika hospitali ya uhuru iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma.

Pamoja na hayo amesema mifumo ya maji na umeme na miundombinu mbalimbali imekamilika pamoja na vifaa tiba vya Utra sound, X-ray,ECG na baadhi ya samani ambavyo vimeshawasili hospitali hapo.

Amesema siku ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar kulifanyika uchangiaji wa damu salama na kufanikiwa kupata unit 48 za damu.

Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe aki akipata maelezo kutoka kwa Mganga mkuu wa halmshauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt.Eusebius Kessy juu ya upatikanaji wa dawa katika chumba cha kuchukulia dawa katika hospitali ya uhuru iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma.

Aidha amelipongeza Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia SUMA JKT ambae ndio mkandarasi wa hospitali iyo,mshauri mwelekezi  wakala wa majengo Tanzania(TBA),Mkurugenzi wa halmashauri ya Chamwino,Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma na Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa usimamizi wa ujenzi wa hospitali hiyo.

Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akimjulia hali mgonjwa aliyefika kupata matibabu katika hospitali ya Uhuru iliyokamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma. Kushoto ni Mganga mkuu wa Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt.Eusebius Kessy.Picha na MAELEZO

Lengo la ujenzi wa Hospitali ya chamwino ni kuboresha huduma za kijamii Dodoma ikiwamo afya ili kutimiza azma ya Serikali kuhamia Dodoma ambayo ndio makao makuu ya nchi.

Ujenzi wa Hospitali ya Chamwino ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwamba Fedha  zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania bara za tarehe 9 desemba 2018 zitumike kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Chamwino.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *