DKT. NDUGULILE AWATAKA TTCL KUONGEZA UBUNIFU NA UTAFITI WA MASOKO YA HUDUMA NA BIDHAA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akifunga kikao cha Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amefunga kikao cha Mameneja wa Mikoa yote ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kilichofanyika Dodoma kwa muda wa siku tatu ambacho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi, Menejimenti ya Wizara na wa TTCL na wawakilishi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (hawapo pichani) wakati wa kikao cha utendaji wa Shirika hilo kilichofanyika Dodoma. Anayesikiliza kwa makini ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba

Dkt. Ndugulile ameipongeza TTCL kwa kujiwekea malengo ya kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo na kuazimia kuongeza idadi ya wateja kutoka asilimia 2 hadi asilimia 6 kwa mwaka mmoja wanaotumia simu za mkononi waliopo kwenye soko; kuongeza idadi ya mawakala wa vocha na wa huduma za fedha mtandao za T – PESA kutoka 2,800 hadi 3,080 katika kipindi cha miezi mitatu; na kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wateja

Ad
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akifafanua jambo wakati wa kufunga kikao cha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) na Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula

Amesema kuwa imejitokeza tabia ya baadhi ya taasisi za umma kutumia huduma za TTCL bila kulipa na amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba kuziandikia taasisi zinazodaiwa kuwa walipe madeni yao vinginevyo ifikapo tarehe 31 Januari, 2021 wazikatie huduma hizo  

Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania wa mikoa yote wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia na Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati akifunga kikao cha Mameneja hao kilichofanyika Dodoma

Ameilekeza TTCL kuchukua hatua kwa watu wanaohujumu miundombinu ya TEHAMA ya TTCL na kudhoofisha ubora wa huduma zake; kuboresha mifumo ya kuhudumia wateja ili kuongeza imani ya wateja kwa Shirika; kuangalia upya mikataba inayoigharimu Shirika ambayo imesainiwa baina ya TTCL na watoa huduma; wajiandae kuingia mikataba baina ya Wizara na Mkurugenzi Mkuu wao na Mameneja ili kupima utendaji kazi; na waongeze ubunifu na kufanya utafiti wa masoko ya huudma za bidhaa zinazotakiwa na wateja

Meneja Kituo cha Biashara Pemba wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Khamis Ngwale akimshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula kwa niaba ya Mameneja wa Shirika hilo baada ya kutoa neno la shukrani kwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto) baada ya kufunga kikao cha Mameneja hao, Dodoma. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi

Na Prisca Ulomi,WMTH

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa Wizara na taasisi tukipanga kwa pamoja inakuwa rahisi kuratibu, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa malengo na maazimio tuliyojiwekea ya kuhudumia wananchi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameikumbusha TTCL kuhakikisha kuwa wanajali mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa TTCL ili kuwaongezea ari, morali na motisha ya kuwahudumia wateja

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema kuwa wamejipanga kutekeleza maazimio na malengo waliyojiwekea ili kuomgeza huduma na bidhaa za mawasiliano kwa wananchi

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *