BALOZI IBUGE AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWANANSHERIA MKUU WA ZANZIBAR

Na Nelson Kessy, Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akutana na kufanya mazungumzo na Mwanansheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji katika Afisi za Mwanasheria Mkuu mjini Zanzibar

Ad
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge  akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu Zanzibar

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya kazi baina Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge  akiongea na Mwanansheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu Zanzibar

Balozi Ibuge amesema kuwa jukumu kubwa la watendaji wa Serikali hizi mbili ni kuhakikisha wanatekeleza maono (vision) viongozi wakuu wa Serikali hasa kwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Ni jukumu letu sisi kama watendaji wa serikali kuwasaidia viongozi wetu kutekeleza maoni ya viongozi wetu kwa kuzingatia Ilani ya CCM ya 2020 – 2025,” Amesema Balozi Ibuge.

Mwanansheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji akimkabidhi moja ya zawadi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge

Kwa upande wake Dkt. Mwinyi Talib Haji amemuahidi Balozi Ibuge kuwa wataendelea kushirikiana katika kuhakikisha kuwa malengo ya serikali zote mbili yanatekelezwa kwa maslahi mapana ya pande zote mbili. “Nakuahidi kuwa sisi kama Afisi ya Mwanasheria Mkuu – Zanzibar tutashirikina na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha tunatekeleza majukumu ya serikali,” Amesema Dkt. Haji.

Mwanansheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mambo ya Nje – Zanzibar Bw. Masoud Balozi Masoud (kushoto) pamoja na Msaidizi wa Katibu Mkuu Bw. Hangi Mgaka (kulia) 
Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *