WAZIRI MKUU ACHANGISHA SH. MILIONI 18.9 KUMSAIDIA MTOTO MIRIAM

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameendesha harambee ya papo kwa papo na kuchangisha sh. milioni 18.9 ambapo kati ya hizo, sh. milioni 10 zimetolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akifuatilia tukio hilo kupitia Televisheni.

Fedha hiyo ilichangishwa kwa ajili ya Miriam Msagati, binti mwenye ulemavu wa mwili ili ziweze kumsaidia kama mtaji wa biashara na uendelezaji wa ujenzi wa vyumba vya kupangisha katika nyumba ambayo amekabidhiwa leo (Ijumaa, Januari 22, 2021) na Waziri Mkuu. Gharama ya ujenzi wa nyumba na samani zilizomo ndani ni sh. milioni 47.32.

Ad

Waziri Mkuu ameendesha harambee hiyo kwenye kitongoji cha Fune, kata ya Mombo wilayani Korogwe baada ya kumkabidhi binti huyo nyumba aliyojengewa na wadau mbalimbali kutokana na mchango ulioasisiwa na Waziri Mkuu Machi 5, 2020 alipomtembelea Miriam na kumpatia mchango wa sh. milioni 5 za kuanza ujenzi wa nyumba hiyo.

Akiwa bado anaendesha harambee hiyo, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan alizungumza na wananchi hao kupitia simu aliyompigia Waziri Mkuu, ambapo alimpongeza kwa kuhakikisha Miriam anapata makazi bora.

 “Nimeona kazi kubwa iliyofanyika hapo, hongereni sana Waziri Mkuu pamoja na uongozi wa mkoa wa Tanga nami namuongezea shilingi milioni tano afanye mtaji.” Amesikika Mama Samia.

Kwa upande wake, Miriam baada ya kukabidhiwa nyumba hiyo alimshukuru Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia, Waziri Mkuu kwa uongozi wao wenye kujali wanyonge. Amesema Tanzania imepata kiongozi mzuri anayewajali wanyonge, hivyo ameahidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awazidishie baraka ili wapate mafanikio mazuri zaidi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *