DK. AKWILAPO AIPONGEZA CSSC KWA KUTOA ELIMU BORA NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk.Leonard Akwilapo, ameipongeza Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii(CSSC),kwa mchango wake katika sekta ya elimu nchini huku akiahidi serikali kufanyia kazi maoni yanayotolewa ikiwamo kupunguza kwa mitihani ya majaribio.

Akifungua leo Mkutano wa mwaka cha Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi za makanisa, Dk.Akwilapo, amesema suala la mitihani ya majaribio lina utata na kudai kuwa ni mingi na wakati mwingine inaipa Wizara wakati mgumu kuiratibu.

Ad

“Kuna wengine wanadhani elimu inapatikana kwa kuuliza wanafunzi maswali mara kwa mara, ili ng’ombe anenepe ni kuhakikisha amekula na si kumpima uzito asubuhi, mchana na jioni, kitu kizuri ni kuimarisha ufundishaji,”amesema.

Ameongeza kuwa “Kuna dhana nyingine imeongezeka hadi kuweka kambi kufanyishwa mitihani kila siku hadi jumamosi,kuna mambo tumekemea na si sahihi kwamba ili mwanafunzi afaulu ni kupigwa mitihani, majaribio hatuyakatai bali kila mara inamchosha mtoto.”

Aidha, amesema nia ya serikali ni kutoleta mgongano na wanaendelea na majadiliano na kutaka kuimarisha ufundishaji na si kupewa mitihani kila siku.

Pia amezitaka shule kuzingatia maelekezo ya serikali katika kumkaririsha mwanafunzi darasa kwa kuwa suala hilo linalalamikiwa.

“Tunatambua mchango wenu mnaoutoa nchini katika sekta ya elimu, hata hivyo baadhi ya shule zisizo za serikali kama nyingine zipo kwenu au hazipo, ambazo zinaenda kinyume na maelekezo ya serikali, niwakumbushe myazingatie kukaririsha wanafunzi bila kuzingatia taratibu ni tatizo tunalokutana nalo sana,”amesema.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume hiyo, Peter Maduki, amesema la mkutano huo ni kuweka mikakati ya utoaji huduma bora ya elimu na kuangalia kero zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

“Pia tutajadili namna ya kuboresha huduma ya  TEHAMA itatusaidia sana katika kuboresha elimu na kupunguza gharama ya utoaji wa elimu na kuwapunguzia mzigo wazazi,”amesema.

Ameomba Wizara kuangalia namna ya kupunguza mitihani ya majaribio ambayo imeonekana kuendelea kuibuka mbali na inayopaswa kufanyika kitaifa.

“Kunaendelea kuibuka mitihani ya majaribio mara ya kikata, kiwilaya hali inayosababisha mwingiliano wa mitihani na hii hata inashusha ubora wa mitihani tunaomba umakini zaidi uwepo katika kuendesha mitihani,”amesema.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Awakaribisha Wawekezaji Katika Nishati ya Jotoardhi Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewakaribisha wawekezaji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *