NAIBU WAZIRI BYABATO AITAKA TANESCO ISHIRIKIANE NA MBUNIFU WA MTAMBO WA KUFUA UMEME KWA KUTUMIA SUMAKU KUTENGENEZA MTAMBO MWINGINE MPYA

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akisoma kipimo cha umeme kinachotumika kupima kiwango cha umeme kinachozalishwa kwenye mtambo wa kufua umeme kinachoitwa (Clamp digital meter) kipimo hicho kimethibitisha kuwa, umeme unaozalishwa na mtambo uliobuniwa na Mbunifu Rojers Msuya unakidhi viwango vyote vya TANESCO.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato, ameiagiza TANESCO kushirikiana na Mbunifu wa Mtambo wa Kufua umeme kwa kutumia sumaku kutengeneza Mtambo mwingine mpya ndani ya wiki mbili.

Naibu Waziri Byabato ametoa maelekezo hayo leo tarehe 25 Januari, 2021 alipomtembelea Mbunifu huyo Bw. Rojers Msuya (52) nyumbani kwake Kawe, jijini Dar-es-salaam kushuhudia ubunifu wake wa kutengeneza mtambo wa kufua umeme kwa kutumia sumaku baada ya kupata taarifa kuhusiana na mbunifu huyo.

Ad
Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akipata maelezo kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Umeme wa Wizara ya Nishati, Mha. Innocent Luoga, kabla ya kukutana na Mbunifu wa ufuaji umeme kwa kutumia sumaku. Aliye kati ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji – Usafirishaji wa TANESCO Isaac Chanji (akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO)

Naibu Waziri Byabato amesema, gharama zote za kutengeneza Mtambo huo, zitagharamiwa na Serikali kupitia shirika lake la TANESCO.

Naibu Waziri Byabato ameelezea kufurahishwa kwake na ubunifu huo na kusema kuwa kufanikiwa kutengeneza mtambo wenye uwezo mkubwa wa kufua umeme kwa kutumia sumaku kutawezesha maeneo ambayo bado hayajafikiwa na umeme wa TANESCO na REA kupata umeme kwa gharama nafuu.

Rojers Msuya (52) Mkazi wa Kawe, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar-es-salaam ambaye ni Mbunifu wa Mtambo wa kufua umeme kwa kutumia sumaku akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 25 Januari, 2021 nyumbani kwake Kawe jijini Dar-es- salaam mara baada ya Kutembelewa na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato.

Naibu Waziri Byabato amemhakikishia Bw. Rojers Msuya kuwa, teknolojia ya kutengeneza mtambo wa kufua umeme kwa kutumia sumaku ikifanikiwa, atahakikisha Haki miliki zake zote kuhusiana na ugunduzi huo zinalindwa na kuhakikisha kunakuwepo na mikataba ya kisheria katika kushirikiana na TANESCO katika kutengeneza mitambo hiyo.

Naye Mbunifu huyo wa Mtambo wa kufua umeme kwa kutumia sumaku Bw. Rojers Msuya, amemweleza Naibu Waziri Byabato kuwa, Mtambo alioutengeneza una uwezo wa kuzalisha KVA 5 sawa na WATT 5000 na kuwa endapo atapata ushirikiano kutoka Serikalini itawezesha kupanua teknolojia hiyo aliyoibuni ya kufua umeme kwa kutumia sumaku.

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji – Usafirishaji wa TANESCO Isaac Chanji (akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO). Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Umeme wa Wizara ya Nishati, Mha. Innocent Luoga, mara baada ya kuwasili Kawe jijini Dar-es-salaam kwa lengo la kukutana na Mbunifu wa ufuaji umeme kwa kutumia sumaku.

Na Dorina Makaya – Dar-es-salaam.

Bw. Rojers amemweleza Naibu Waziri Byabato kuwa, hadi sasa, tayari amekwishatengeneza mashine 10 za majaribio za kufua umeme kwa njia ya sumaku na kuwapatia watu mbali mbali kuifanyia majaribio mitambo hiyo na hakuwahi kupata malalamiko yoyote kutoka kwa watumiaji hao kwa kipindi cha miaka minane sasa.

Bw. Rojers amesema sifa za Mitambo hiyo aliyoibuni ni kuwa haina kelele, haichafui mazingira na inaweza kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 bila ya kufanyiwa matengenezo.

Bw. Rojers amemshukuru Naibu Waziri Byabato pamoja na viongozi wengine wa Wizara ya Nishati na TANESCO kwa kumtembelea na kujionea ubunifu wake.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato, aliambatana na Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mha. Innocent Luoga (aliyemwakilisha Kamishna wa Umeme Wizara ya Nishati), Naibu Mkurugenzi Mtendaji – Usafirishaji wa TANESCO, Mha. Isaac Chanji (aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO), Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO pamoja na timu ya Waandishi wa Habari.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *