DC CHONGOLO APOKEA RIPOTI YA CHANGAMOTO YA TOPE KUTOKA KWA WATAALAMU WA JIOLOJIA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amepokea ripoti  ya utafiti iliyofanywa na wataalamu wa Jiolojia kuhusiana na kuwepo kwa changamoto ya Tope katika eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana.

Mhe. Chongolo ampokea taarifa hiyo leo ofisini kwake kutoka kwa Timu ya wataalamu iliyokuwa inacunguza changamoto hiyo ikiongozwa na Mhadhiri wa Jiolojia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Remigius Gamba, ambaye ndio kiongozi mkuu wa kamati hiyo.

Ad
Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa madini Tanzania  bwana Maruvuko Msechu akiwasilisha Taarifa ya ripoti ya changamoto ya Tope  iliyotokea Kunduchi Jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana.

Akizungumza mara baada ya kupokea kwa taarifa hiyo, Mhe. Chongolo ameeleza kuwa mara baada ya kutokea kwa changamoto hiyo, Serikali ilichukua hatua ya  kuunda kamati ya wataalamu kwa ajili ya kuchunguza hali hiyo na hivyo kuipongeza kutokana na kazi kubwa waliyoifanya.

Mhe. Chongolo ametaja watalamu waliohusika katika utafiti wa changamoto hiyo kuwa ni kutoka  Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa madini Tanzania (AGST), Chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia shule ya migodi na madini idara ya Jiosayansi, Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) pamoja na  Chuo cha mafunzo ya Jiosayansi (AMGC).

Wajumbe wa kamati pamoja na watalamu waliohusika katika utafiti wa changamoto ya Tope iliyotokea Kunduchi Jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana.

Ameongeza kuwa kupitia ripoti hiyo, ushauri uliotolewa na wataalamu hao utafayiwa kazi kwa pamoja kama Serikali kuanzia ngazi ya wilaya hadi ile ya juu inayohusiana na uchakataji wa taarifa pamoja na utekelezaji wake.

Hata hivyo Mhe.Chongolo amesema kuwa utafiti huo ulikuwa ukifanyika kwa kushirkiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Abuubakari Kunenge na kwamba kutokana na umuhimu huo ataiwasilisha kwakwe ili aweze kujua matokeo ya kamati hiyo.

Hata hivyo Mhe. Chongolo amewataka wananchi kuacha kusikiliza taarifa zisizo rasmi kutoka katika vyanzo mbalimbali na badala yake wasikilize na kufuata maelekezo yatakayotolewa na  Serikali kupitia watalaamu wake.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *