DKT. NDUGULILE AJIKITA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAWASILIANO YA SIMU NA DATA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na Watendaji Wakuu wa Makampuni ya simu nchiniwengine kutoka kulia ni katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, wengine kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula, Naibu wake dkt Jim Yonazi na Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Clarence Ichwekeleza.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake inashirikiana na wadau wa sekta ya mawasiliano kuhakikisha inatatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili wananchi waweze kupata huduma bora za mawasiliano kwa gharama nafuu katika maeneo yote nchini.

Amezungumza hayo katika kikao chake cha majadiliano na Watendaji Wakuu wa makampuni ya simu Tanzania kilichofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma kwa lengo la kutatua changamoto na kuwa na mkakati wa pamoja wa kuongeza wigo wa mawasiliano ya kasi ya simu na data nchini.

Ad
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Zainab Chaula akizungumza katika kikao cha Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) na Watendaji Wakuu wa Makampuni ya simu nchini (hawapo pichani),wengine kulia ni Naibu wake Mhandisi Andrea Kundo, wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu Dkt Jim Yonazi na Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Clarence Ichwekeleza.

Ndugulile amesema kuwa matamanio ya Serikali ni wananchi wake kuweza kutumia mawasiliano ya simu na data kufanya biashara mtandao, kupata huduma mbalimbali za Serikali kwa njia ya mtandao na kushiriki katika kuinua uchumi wa kidijitali.

“Tumefanya kikao cha ndani na Watendaji Wakuu wa makampuni ya simu na kuongelea masuala ya vifurushi na bando, suala hili tunalifanyia kazi kwa pamoja na hivi karibuni Serikali itatoa tamko kuhusiana na masuala ya vifurushi”, amezungumza Ndugulile

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Andrea Kundo (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi James Kilaba wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Makampuni ya simu, jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na watoa huduma za mawasiliano nchini kwa kuhakikisha inatengeneza mazingira wezeshi na kutatua changamoto zinazojitokeza katika sekta ya mawasiliano.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Zainab Chaula alisema kuwa Serikali imewekeza katika TEHAMA ili kuwezesha na kuboresha uzalishaji na uendeshaji wa sekta takribani zote nchini, na kuwataka wadau wa sekta ya mawasiliano kutembea pamoja ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuipeleka nchi katika mapinduzi ya nne ya viwanda na uchumi wa kidijitali.

Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Makampuni ya Simu nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile, wakati wa kikao chake na watendaji hao, jijini Dodoma

Na Faraja Mpina – WMTH

Naye Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba amesema Mfuko huo umeratibu kikao hicho cha wadau wa mawasiliano ikiwa ni agizo la Mhe. Waziri, ambapo moja ya ajenda ni kufanya majadiliano ya namna bora ya kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini na mipakani kwa kutumia teknolojia bora na rahisi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *