TBS YATEKETEZA BIDHAA ZISIZOKIDHI UBORA ZENYE THAMANI YA MILIONI 40

Na Eliud Rwechungura

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa zisizokidhi ubora wa viwango yenye thamani ya shilingi milioni 40 ambazo ziliondolewa sokoni na Wakaguzi wa TBS kanda ya kati kuanzia mwezi Novemba, 2020 hadi Januari 15, 2021.

Zoezi hilo la uteketezaji bidhaa hizo limefanyika katika dampo Chidachi – Dodoma, Januari 27,2021

Bidhaa zilizoharibiwa ni pamoja na vipodozi vyenye viambata sumu, vyakula na vinywaji ambavyo muda wake wa matumizi umepita (Expired produducts) vilivyopatikana katika maduka mbalimbali yaliyopo katika mikoa ya Dodoma, Tabora na Singida.

Bidhaa za vipodozi vyenye viambata sumu, vyakula na vinywaji ambavyo muda wake wa matumizi umepita (Expired produducts) zisizokidhi ubora wa viwango yenye thamani ya shilingi milioni 40 ambazo ziliondolewa sokoni na Wakaguzi wa TBS kanda ya kati na kuteketezwa  katika dampo la Chidachi Dodoma, Januari 27,2021 (Picha na Eliud Rwechungura)

Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009 pamoja na Sheria ya Fedha Na.8 ya mwaka 2019 mbali na majukumu mengine zimelipa mamlaka Shirika kuondoa bidhaa hafifu sokoni na kuziharibu ama kuzirudisha zinakotoka pindi zinapobainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Wakaguzi wa TBS hufanya ukaguzi wa bidhaa wa bidhaa viwandani na sokoni ili kujiridhisha na hali halisi ya soko na inapobainika uwepo wa bidhaa hafifu huondolewa sokoni na aliyekutwa na bidhaa hizo hulazimika kulipia gharama ya uteketezaji.

Mkaguzi wa udhibiti ubora TBS, Lazaro Msasaranga ametoa rai kwa wafanyabiashara wote kuhakikisha kuwa wakati wote wanazingatia masuala ya ubora kwa kuuza bidhaa za vipodozi na vyakula vilivyosajiriwa pamoja na ukomo wa matumizi wa bidhaa hizo ili kumulinda mlaji na kuepuka hasara ya kuharibiwa bidhaa hizo. Pia wafanyabiashara wote wanatakiw kusajili bidhaa za vyakula, vipodozi, majengo ya kufanyia biashara na maghara ya kuhifadhia bidhaa hizo.

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.