RAIS MAGUFULI AMEIPANDISHA HADHI HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA KUWA MANISPAA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Chapulwa Kahama mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha Nafaka, Vinywaji na Maziwa (Kom Limited) Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Januari 2021.

Rais Dkt. John Magufuli ameipandisha hadhi Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga kuwa Mansipaa ya Kahama, Rais Magufuli amesema hayo akiwa anazungumza na wananchi wa wilaya ya Kahama mkoani humo.

Rais Magufuli yupo kwenye Ziara ya kikazi mkoani humo ambapo ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha vinywaji baridi, nafaka na vifungashio cha KOM Food Products na pia ameweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Halmashauri ya mji wa Kahama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mawaziri, pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Shinyanga akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha Nafaka, Vinywaji na Maziwa (Kom Limited) Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Januari 2021. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza kufanya kazi Mwezi Julai mwaka huu.
Baadhi ya viongozi mbalimbali pamoja na wabunge wakipiga makofi mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza kumsamehe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson David Msumba (aliyesimama)ambaye alikuwa miongoni mwa Wakurugenzi wachache walionunua Magari ya Kifahari tofauti na maagizo ya Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telak ili aweze kumsaidia Mama Cristina Masigwa ambaye anadai kudhulumiwa kipande cha Ardhi mkoani Shinyanga.
Picha namba 12. Mama Cristina Masigwa akizungumza kuhusu kero yake ya kudhulumiwa kipande cha Ardhi mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu. PICHA NA IKULU

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.