BALOZI BRIGEDIA GENERALI IBUGE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI LUVANDA

Balozi Brigedia Generali Wilbert Ibuge,Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Baraka Luvanda Balozi wa Tanzania nchini India katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.  

Mazungumzo hayo yalilenga kubadilishana mawazo na uzoefu baina yao kuhusu masuala mbalimbali hususan katika kudumisha na kuboresha uhusiano na ushirikiano uliopo katika ya Tanzania na India, kutangaza fursa zilizopo Tanzania ili kuvutia zaidi biashara na uwekezaji nchini kutoka India. 

Ad
Balozi Brigedia Generali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Baraka Luvanda Balozi wa Tanzania nchini India wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.

 Jitihada za kutangaza fursa zinazopatikana nchini zimekuwa zikiendelea kufanywa na Wizara, kupitia Balozi zake ikiwa ni utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha kuwa Diplomasia ya Uchumi inatekelezwa ili kuinufaisha nchi kupitia fursa zilizopo. 

Balozi Brigedia Generali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na Mhe. Baraka Luvanda Balozi wa Tanzania nchini India alipowasili Wizarani kufanya mangumzo na Katibu Mkuu.

Tanzania na India zimekuwa na ushirikiano mzuri na wakudumu wa kidipolomasia na kiuchumi ambao umeendelea kuzinufaisha nchi zote mbili. Mfano, Juni 2015 Tanzania ilinufaika na mkopo kutoka nchini India wa upanuzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Vikitoria kwenda Mkoani Tabora, mradi huu ambao unanufaisha zaidi ya watu 1,433,004 ulikamilika mwaka 2019. 

India ilianzisha Ubalozi wake nchini Tanzania mwaka 1961 (wakati huo ilijulikana kama Tanganyika), hii ilikuwa kabla Tanganyika haijapata uhuru, na Tanganyika ilianzisha Ubalozi wake nchini India mwaka 1962, mara baada ya kupata Uhuru.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME MWANGA KOROGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba yaMungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024. Makamu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *