NAIBU WAZIRI WA MAJI AZINDUA MRADI WA MAJI KWIMBA MKOANI MWANZA

Naibu Waziri Maryprisca Mahundi akimtua ndoo mama kichwani katika kijiji cha Mwabaratulu Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ikiwa ni ishara ya kumalizwa kero ya maji katika Kijiji hicho.

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi  Maryprisca Mahundi (Mb)amezindua mradi wa maji Kijiji cha Mwabaratulu Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ulioghalimu shilingi milioni 177.

Aidha wananchi wamepewa mwezi mmoja kutumia maji bure bila malipo.


Hata hivyo Naibu Waziri amewataka kutunza miundo mbinu ya maji ili serikali ifikie malengo yake sambamba na kumtua mama ndoo kichwani kwani wanawake ndiyo wahanga wakubwa ikiwa ni pamoja na migogoro katika ndoa.

“Mheshimiwa Rais Magufuli ametoa pesa nyingi katika miradi ya maji nchini hivyo wataalamu na wananchi tunapaswa kushirikiana ili kuifikia matamanio ya Rais kuona kila Mtanzania anakunywa maji safi na salama” alisema Naibu Waziri wa Maji.

Ad


 

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *