Halmashauri ya Chalinze yakabidhi Viti-Mwendo 10 kwa watoto wenye Ulemavu.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete amewashukuru watendaji wa Halmashauri kwa utekelezaji wa maagizo yanayotolewa kwenye vikao.
Mbunge Kikwete amepongeza hatua hiyo ya kufikia malengo ya Serikali ya kuhakikisha kila mtoto wa Tanzania anakwenda shule kama alivyoelekeza na Rais Dkt. John Magufuli.
Kikwete alieleza kufurahishwa na hatua hiyo ya halmashauri kununua vifaa hivyo kwa kutumia mapato ya ndani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi amesema kuwa Halmashauri imejipanga kujenga mabweni kwa ajili ya watoto katika kata ya Kiwangwa na Bwilingu ili kuongeza ari ya kuhakikisha watoto wanasoma.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameelezea changamoto ya uhaba wa walimu na kuomba serikali kuongeza idadi ya walimu katika Halmashauri hiyo.