MAHINDI YA TANZANIA NI SALAMA KWA MATUMIZI YA BINADAMU NA WANYAMA, NA YANAKIDHI VIGEZO VYOTE VYA KIMATAIFA – BASHE

Ameandika Naibu Waziri Hussein Bashe kuhusu mahindi ya Tanzania:

Salaam Ndg. zangu nataka niseme kuwa Mahindi ya Tanzania ni Salama kwa matumizi ya Binadamu na Wanyama,na yanakidhi vigezo vyote vya Kikanda na kimataifa.

Ad

Biashara ni suala la hiari, wanaweza kununua au kutonunua kutoka kwetu. Kinachotusumbua sisi ni kauli ya upotoshaji ya Wizara ya Kilimo ya Kenya. Sisi Tanzania tunafanya Biashara ya Mahindi na Mataifa na taasisi za kimataifa na inaendelea.

Nataka kuwahakikishia kuwa Tunaendelea na Mazungumzo Kama mwanachama wa EAC ili kufikia maelewano ya KUHESHIMIANA.

Hata sampuli walizochukua Shirika la Viwango la Kenya – KEBS katika mpaka wa Horohoro siku ya Jumamosi matokeo hayakua kama ambavyo Kenya walivohubiria Dunia. Tunawasihi wenzetu, jirani zetu na ndugu zetu Kenya watumie njia sahihi za malalamiko.

Tanzania Tunaendelea kuuza Mahindi maeneo mengine kama DRC,Burundi,Rwanda na Sudan Kusini. Taasisi Kama WFP inanunua Mahindi na kesho kupitia Bandari ya Kasanga Mkoa wa Rukwa watapakia Meli yenye Tani 300 za Mahindi kuelekea Bujumbura, Burundi. Mahindi yetu ni salama.

Tunasisitiza kuwa Afflatoxine levels na Moisture level ya Mahindi ya Tanzania ambayo tunatumia ndani na tunayouza nje yanakidhi vigezo vya kimataifa Tusiwe na hofu tunafanya majadiliano kufikia Muafaka utakao jenga kuheshimiana.

Ni dhahiri Kuwa EAC inafahamu ni nchi gani inaongoza kwa SUMUKUVU. Ieleweke biashara ni hiari lakini Upotoshaji hautavumilika.
Tutaendelea kufata njia za kidiplomasia kumaliza Jambo hili. Tunalichukulia kwa Uzito unao stahili ni wajibu wetu kutetea maslahi ya Watanzania.

Asanteni sana

H. M . Bashe
Naibu Waziri wa Kilimo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *