WAZIRI WA FEDHA DKT. MWIGULU NCHEMBA NA NAIBU WAKE MHANDISI MASAUNI WAANZA KAZI RASMI BAADA YA KUAPISHWA

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Bi. Emiliana Shayo, alipowasili katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Kiserikali wa Magufuli -Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Maganga na viongozi wengine wa Wizara. Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Bi Amina Shaabani, Kamishna wa Fedha za Nje, Bi. Sauda Msemo (wa pili kushoto), alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James, alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James, wakati wa kikao cha menejimenti ya wizara kilichofanyika Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu, Bw. Doto James, baada ya kupokea nyaraka mbalimbali, wakati wa kikao cha menejimenti ya wizara kilichofanyika Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akizungumza na viongozi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), wakati wa kikao cha menejimenti katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma ambapo aliwahimiza kufanya kazi kwa ushirikiano kwa maslahi ya Taifa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akizungumza jambo na viongozi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha menejimenti katika Ofisi za Wizara Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika kikao cha menejimenti ya wizara katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *