KATIBU MKUU NZUNDA AHIMIZA KASI NA MATOKEO CHANYA OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya akiweka saini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) amewataka Manaibu Makatibu Wakuu wapya, Menejimenti  na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza kasi, bidii na ari katika utendaji kazi wa majukumu ili kutoa matokeo yenye tija  kwa wananchi.

Katibu Mkuu Nzunda ameyasema hayo leo tarehe 8 Aprili, 2021, Jijini Dodoma, wakati wa kuwapokea Manaibu Makatibu Wakuu wapya wa Ofisi ya Waziri Mkuu walioapishwa Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Aprili 6, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Ad
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper K. Mmuya akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili na kupokelewa na watumishi hao katika ofisi zao zilizopo Mtumba Dodoma.

Ameeleza kuwa, Ofisi hiyo ina majukumu makubwa ikiwemo kuratibu shughuli za Serikali, hivyo ni muhimu kuongeza nguvu zaidi katika utekelezaji wa majukumu ili kusimamia kwa ufanisi uratibu wa shughuli za serikali.

“Jukumu letu ni kumsaidia Mhe. Waziri Mkuu kutekeleza majukumu ya kusimamia shughuli za serikali, hatunabudi kufanya kazi kwa utaalamu, weledi na kwa kuwajibika kwa kujituma ili kuhakikisha matokea anayo yataka,” alisema Nzunda

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akiweka saini katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.

Kwa upande wa Manaibu Makatibu Wakuu wapya; Profesa Jamal Adam Katundu na Kaspar Kaspar Mmuya. wameahidi  kushirikiana na Watendaji wa Ofisi hiyo kumhakikishia  Katibu Mkuu huyo kuwa wapo tayari kufanya kazi kwa  kasi ili kupata matokeo chanya kama ilivyo kusudiwa.

Tarehe 6 Aprili, 2021 Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwaaapisha Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi hiyo

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *