RAIS SAMIA AWATAKA MAWAZIRI NA WATAALAMU WA TANZANIA NA KENYA (JPC) KUKUTANA MARA MOJA ILI KUFANYIA KAZI MASUALA MBALIMBALI YA KUIMARISHA UHUSIANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan tarehe Aprili, 2021 amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Muigai Kenyatta uliowasilishwa na Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi wa Kenya, Balozi Dkt. Amina Mohamed.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta leo tarehe 10 Aprili, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam

Pamoja na kupokea ujumbe huo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Samia amefanya mazungumzo na Mhe. Balozi Amina kuhusiana na dhamira ya Tanzania na Kenya kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali hususani kiuchumi na kijamii.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Kenya hapa nchini Mheshimiwa Dan Kazungu ambaye aliambatana na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta leo tarehe 10 Aprili 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Samia amemhakikishia Rais Kenyatta kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari kuendeleza mambo mazuri yote yaliyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na kutatua changamoto kati ya Tanzania na Kenya kwa kuwa nchi hizi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni ndugu, majirani na marafiki wa kihistoria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta leo tarehe 10 Aprili 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam

Amewataka Mawaziri na Wataalamu wa Tanzania na Kenya wanaounda Kamati ya Ushirikiano wa Pamoja (Joint Permanent Commission – JPC) ambao hawajakutana tangu mwaka 2016 kukutana mara moja ili kufanyia kazi masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta wakwanza kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Athman Kattanga wakwanza (kulia) pamoja Balozi wa Kenya hapa nchini Balozi Dan Kazungu mwenye tai nyekundu, mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Kenyatta amemwalika Rais Samia kufanya ziara rasmi nchini Kenya ili kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano.

Amemhakikishia Rais Samia kuwa Kenya ipo tayari wakati wote kushirikiana na Tanzania kwa kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanahabari mara baada ya kupokea Ujumbe Maalumu kutoka kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Amina ameongozana na Balozi wa Kenya hapa nchini, Dan Kazungu.

Dkt. Amina Mohammed Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuwasilisha Ujumbe huo pamoja na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.
Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *