RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU MZEE ALI HASSAN MWINYI JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alifika kumsalimia Rais Samia Nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Aprili, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo tarehe 12 Aprili, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi ambaye amempongeza kwa kuanza vizuri majukumu yake ya kuongoza nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alifika kumsalimia Rais Samia Nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Aprili, 2021

Akizungumza baada ya mazungumzo yao, Mhe. Rais Mwinyi amesema amefika nyumbani kwa Mhe. Rais Samia kumjulia hali, kumtia moyo na kumhakikishia kuwa yeye na Wazee wenzake wapo tayari kutoa ushirikiano na kumsaidia wakati wowote watakapohitajika kufanya hivyo.

Ad
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Aprili, 2021. PICHA NA IKULU

“Mama ameanza vizuri, ingekuwa ni nyimbo ningesema once more!!!, ameanza vizuri kabisa na kila mmoja ana furaha, kila raia unayemsikia anasema Mama ameanza vizuri, tuliyekuwa nae tulikuwa na Rais mzuri sana, mzoefu wa mambo ya kiserikali, ametufanyia kazi nzuri sana, sasa kaacha mambo haya ghafla kamuachia mwenzie, sasa Mama naye mwanadamu atakuwa na yake na vile vile kuna mambo ambayo yameanzwa na mtu mwingine  ambayo watu wanayataka wanayapenda, wanamshikilia Mama tunayataka haya tunayataka!!, tulieni tutayatekeleza haya, sasa hilo linafurahisha” amesema Mhe. Rais Mstaafu Mwinyi.

Mhe. Rais Mstaafu Mwinyi amewataka Watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Samia kwa kuacha balaa, ugomvi na fitina badala yake wawe na umoja, mshikamano na kufanya juhudi za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *