DAR ES SALAAM SASA WANAJARIBU MAJI, WANAJARIBU KINA CHA MAJI – RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Viongozi wa Kidini, Viongozi Wakuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamesimama wakati wa Wimbo wa Taifa ukipigwa katika ukumbi wa Mlimani City kabla ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipohutubia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Wazee wote nchini kuwa Serikali ya Awamu ya Sita ina dhamira ya dhati ya kushughulikia masuala mbalimbali yanayowahusu ili waweze kuishi maisha mazuri na salama.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo tarehe 07 Mei, 2021 Mkoani Dar es Salaam wakati akizungumza na Wazee wa Dar es Salaam kwa niaba ya Wazee wote wa Tanzania baada ya kupokea risala yao iliyosomwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mzee Salum Abdallah Matimbwa.

Ad

Katika risala hiyo Wazee hao wameomba kutatuliwa changamoto za matibabu, kutungwa sheria ya wazee, kupatiwa fursa za kiuchumi ikiwemo mikopo na misaada, kupatiwa pensheni, kuondolewa kero katika vyombo vya usafiri na kupatiwa nafasi katika vyombo vya maamuzi.

Rais Samia amewashukuru na kuwapongeza Wazee wote wa Tanzania kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika kulilea Taifa kutokana na uzoefu na ujuzi walionao na pia amewashukuru kwa pongezi za kupokea kijiti cha Urais na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara, Philip Mangula, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mkutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021.

Amewaahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itajitahidi kushughulikia changamoto walizozitaja kulingana na uwezo wa kifedha utakavyoruhusu lakini amemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kushughulikia kwa haraka changamoto ya matibabu ya Wazee nchini kote.

Kuhusu pensheni kwa Wazee wote amesema kulingana na hali ya uchumi kwa sasa Serikali haitaweza kutekeleza ombi hilo mpaka hapo hali ya uchumi itakapoimarika lakini amesema imejipanga kuwawezesha Wazee kupitia mradi wa kusaidia kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) na kwamba baada ya kuisha kwa mradi unaoendelea hivi sasa Serikali inajipanga kuendeleza mradi huo ili uwafikie wazee wote nchini.

Pamoja na kukubali kuwa Serikali itaimarisha nyumba za Wazee, Mhe. Rais Samia ametoa wito kwa jamii kuendeleza utamaduni mzuri wa kuwatunza wazee vizuri na kwa upendo majumbani badala ya kuwaweka kwenye vituo vya wazee.

Viongozi wa Kidini, Viongozi Wakuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamesimama wakati wa Wimbo wa Taifa ukipigwa katika ukumbi wa Mlimani City kabla ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipohutubia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, ametoa wito kwa Wazee hao na Wazazi wote nchini kuwalea vijana wao katika maadili mema ili watambue wajibu wao kwa Wazee, nidhamu na heshima kwa jamii na kuwajali Wazee wote hasa wanapotumia huduma za kijamii ikiwemo mabasi ya abiria na sehemu za kutolea huduma.

Ameonya dhidi ya vitendo vya ujambazi na wizi vilivyoanza kujitokeza katika Mkoa wa Dar es Salaam na amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IJP-Simon Sirro kudhibiti vitendo hivyo mara moja.

Viongozi wa Kidini, Viongozi Wakuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiomba Dua kabla ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipohutubia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Rais Samia amesema katika kutekeleza vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita anatarajia kuendeleza kazi nzuri iliyofanyika katika awamu zote za uongozi zilizopita, kumtumia Mtanzania yeyote mwenye ujuzi na maarifa ya kufanya kazi na atayeonekana anafaa ilimradi asiwe na dosari za kimaadili na usalama, na kutokana na hilo atafanya mabadiliko ya kitaasisi na uongozi kadiri atakavyoona inafaa kwa nia njema ya kulipeleka Taifa mbele.

Sehemu ya Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam

Ameupongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukaribia kumaliza kabisa kero ya maji baada ya kukamilika kwa miradi miwili ya maji, ameahidi kuendeleza juhudi za kuongeza uzalishaji wa umeme ili utumike kuendeleza viwanda na kuuza nje ya nchi, kuongeza kasi ya kupanua huduma za mawasiliano kupitia mkongo wa Taifa, kusimamia uhuru, haki na demokrasia na kukuza uhusiano na ushirikiano na Mataifa mbalimbali duniani kama alivyofanya hivi karibu katika ziara yake rasmi nchini Kenya.

Rais Samia amewaomba Wazee wote nchini kumuunga mkono na kuwakumbusha Watanzania wote wajibu wao wa kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, kulipa kodi na kusimamia maadili ya Kitanzania.

Mkutano huo umehudhuriwa na Makamu wa Rais Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula, Viongozi wa Dini na viongozi wa vyama vya siasa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME MWANGA KOROGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba yaMungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024. Makamu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *