TANZANIA KINARA WA UBORA WA SEKTA YA FEDHA KUSINI MWA AFRIKA

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. FLorens Luoga, wakisikiliza mada mbalimbali kuhusu masuala ya Fedha na uchumi wakati wa Semina kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, iliyofanyika Zanzibar.

Sekta ya Fedha nchini Tanzania inaongoza kwa uimara na ubora katika nchi za Kusini mwa Bara la Afrika na Afrika Mashariki kwa vigezo vyote kutokana na usimamizi madhubuti wa uchumi na maboresho ya sekta hiyo.

Hayo yamebainishwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. FLorens Luoga, wakati wa Semina kuhusu masula ya Fedha na uchumi kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, iliyofanyika Zanzibar.

Ad

Prof. Luoga alisema kuwa Benki Kuu inajivunia mafanikio makubwa katika mageuzi na maboresho ya Sekta ya Fedha ambayo yameifanya Sekta kuwa tulivu na kuwafanya wawekezaji kuwa na Imani zaidi ya kuwekeza nchini.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Semina kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Semina iliyoendeshwa na Benki hiyo, Zanzibar.

“Kutokana na uimara wa Sekta ya Fedha, Tanzania inashika nafasi ya tatu Barani Afrika kwa vigezo vya kukopesheka ikitanguliwa na Nigeria na Ethiopia na haya ni matokeo ya usimamizi thabiti wa uchumi wa nchi”, alieleza Prof. Luoga.

Alisema katika kutekeleza majukumu ya usimamizi wa sekta ya fedha, kuna umuhimu wa kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na wadau, wakiwemo Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili kufikia malengo yanayopangwa hususani katika kufanikisha ukuaji, utulivu na ustawi endelevu wa sekta ya fedha na uchumi.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. FLorens Luoga (katikati), akifafanua jambo kwa baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, baada yakumalizika kwa Semina kwa Wajumbe hao iliyofanyika Zanzibar.

Alisema kuwa Benki Kuu inayo adhma ya kuendelea kutekeleza majukumu yake makuu ya kudumisha mfumo madhubuti na salama wa fedha na mabenki kwa kupitia usimamizi makini wa mfumo wa malipo wenye usalama na unaoenda na wakati.

Aidha alisema kuwa Semina kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi inalengo la kuwajengea uelewa mpana juu ya majukumu ya BoT pamoja na masuala ya masoko ya fedha hususani Dhamana na Hati Fungani za Serikali.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, alisema kuwa BoT, imefanya tafiti takribani tatu kuhusiana na uchumi wa Blue hivyo ni fursa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuchangia mawazo katika eneo hilo ili kuwezesha kutoa mchango kwa Serikali kwa adhma ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid (katikati), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (wa tatu kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. FLorens Luoga (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na baadhi ya Watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, baada ya Semina kwa Wajumbe hao iliyofanyika Zanzibar.

Na. Peter Haule, WFM, Zanzibar

“Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanalojukumu kubwa la kuisimamia Serikali hususani katika ukuaji wa uchumi, ikizingatiwa kuwa kipaumbele cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi ni kuwepo kwa uchumi wa Blue unaohusu uvuvi hivyo ni vema mkaliangalia kwa kina”, alieleza Mhandisi Masauni.

Mhandisi Masauni, ameipongeza BoT kwa kuandaa Semina kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili kujenga uelewa wa pamoja katika usimamizi wa Sekta ya fedha kwa maendeleo ya Taifa na kukuza uchumi wa wananchi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME MWANGA KOROGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba yaMungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024. Makamu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *