WAZIRI WA UINGEREZA ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA – TANZANIA NI MBIA MUHIMU WA UK NA JUMUIYA YA MADOLA

Uingereza imesema Tanzania ni mbia muhimu wa miaka mingi wa maendeleo na katika Jumuiya ya Madola na kwamba Nchi ya Uingereza itaendelea kushirikiana na Tanzaniakatika masuala ya uwekezaji,biashara,diplomasia na utawala bora.

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge ameyasema hayo katika mazungumzo rasmi aliyoyafanya na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili James Duddridge.

Ad

Mhe Duddridge ameongeza kuwa ziara yake ya siku mbili hapa nchini ina lengo la kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya Uingereza na Tanzania licha ya changamoto ya ugonjwa wa COVID – 19 ambapo Uingereza imekusudia kuisaidia Tanzania kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi,mapambano dhidi ya rushwa lakini pia katika sekta za Afya na Elimu.

Akiizungumzia ziara hiyo ya waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema ziara hiyo ni kielelezo cha Tanzania kuheshimika na kukubalika miongoni mwa Jumuiya za Kimataifa na Mataifa ya nje na kwamba kipaumbele cha Serikali ya awamu ya sita ni diplomasia ya uchumi ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi tatu kubwa zinazowekeza hapa nchini na hivyo kuwa ni miongoni mwa Mataifa muhimu kwa Tanzania……..Balozi Liberata Mulamula 

Balozi Mulamula ameongeza kuwa katika mazungumzo yao msisitizo mkubwa umewekwa katika uchumi na kukuza biashara pamoja na kuiendeleza miradi mikubwa iliyokuwa ikitekelezwa na Uingereza ikiwemo miradi ya kiwanda cha sukari na madini. 

Balozi Mulamula ameongeza kuwa ujio wa Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge hapa nchini inathibitisha kuwa mahusiano ya Tanzania nje ya mipaka yake bado ni imara licha ya taarifa potofu zilizokuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya nje zikitilia mashaka juu ya diplomasia ya Tanzania nje ya nchi.

Kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji Balozi Mulamula amemuhakikishia Mhe. James Duddiridge kuwa mazingira ya uwekezaji ni salama na yanavutia baada ya kuboreshwa na hivyo kumtaka kuwahamasisha wawekezaji kutoka Uingereza kuja hapa nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali. 

James kusudio la Tanzania kuendeleza mahusiano mema ya kidiploamsia na ya kiuchumi na mataifa mengine duniani na kumtaka kuhamasisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini Uingereza kuja kuwekeza Tanzania kwakuwa mazingira yameboreshwa 

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME MWANGA KOROGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba yaMungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024. Makamu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *