TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 68 KUTOKA UJERUMANI

Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Tanzania imepokea msaada wa Euro milioni 25 sawa na shilingi bilioni 67.82 kutoka Serikali ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo ya KfW, kwa ajili ya mradi wa Uhifadhi endelevu wa Maliasili na Mifumo ya Ikolojia nchini.

Ad
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) wa Umoja wa Afrika, Bw. Christoph Tiskens, wakisaini Mkataba wa Msaada wa Euro milioni 25 sawa na shilingi bilioni 67.82, kwa ajili ya miradi ya uhifadhi endelevu wa maliasili na mifumo ya ikolojia, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

Mkataba wa msaada huo umesainiwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na  Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) wa Umoja wa Afrika, Bw. Christoph Tiskens, kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani.

Bw. Tutuba alisema kuwa  fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuendeleza na kuhifadhi maliasili katika hifadhi ya Serengeti pamoja na kugharamia mradi wa uhifadhi endelevu wa maliasili na mifumo ya ikolojia katika maeneo ya ushoroba wa Katavi – Mahale.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) wa Umoja wa Afrika, Bw. Christoph Tiskens, wakionesha Mkataba wa Msaada wa Euro milioni 25 sawa na shilingi bilioni 67.82, baada ya kusainiwa, jijini Dar es Salaam.

“Lengo la mradi wa Serengeti ni  kuchangia katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na usimamizi endelevu wa maliasili katika Wilaya ya Bariadi, Bunda, Serengeti na Ngorongoro wakati mradi wa Ushoroba wa Katavi- Mahale unalenga usimamizi wa maliasili sambamba na kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhusisha matumizi bora ya ardhi na utoaji wa Hati miliki za kimila”, alieleza Bw. Tutuba.

Alisema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 21.7 zitatumika katika mradi wa kuendeleza na kuhifadhi maliasili katika hifadhi ya Serengeti na shilingi bilioni 46.12, zitatumika katika mradi wa uhifadhi endelevu wa maliasili na mifumo ya Ikolojia ushoroba wa Katavi – Mahale.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, akielezea malengo ya Msaada wa Euro milioni 25 sawa na shilingi bilioni 67.82, zilizotolewa na Serikali ya Ujerumani kuwa ni uhifadhi madhubuti na endelevu wa maliasili na mifumo ya ikolojia, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess, aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi ambayo hayaiathiri Tanzania pekee bali Dunia kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) wa Umoja wa Afrika, Bw. Christoph Tiskens, alisema kuwa Benki hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania katika Sekta ya Utalii kwa kuboresha maeneo ya hifadhi pamoja na kuziwezesha jamii zinazozunguka maeneo hayo ili waweze kutunza hifadhi hizo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (wa pili kushoto), Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) wa Umoja wa Afrika, Bw. Christoph Tiskens (kulia) na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Sauda Msemo, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania na Ubalozi wa Ujerumanai, baada ya kusainiwa Mkataba wa Msaada wa shilingi bilioni 67.82, kwa ajili ya miradi ya uhifadhi endelevu wa maliasili na mifumo ya ikolojia, jijini Dar es Salaam. (Picha na WFM, Dar es Salaam)

Tanzania imekuwa ikinufaika na ufadhili wa Serikali ya Ujerumani katika sekta ya afya, maji, nishati, matumizi endelevu ya maliasili na usimamizi bora wa fedha za umma ambapo kiasi cha shilingi bilioni 678.54 zilitolewa kwa ajili ya miradi inayoendelea kutekelezwa na shilingi bilioni 599.23 kwa miradi iliyokamilika.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

107 Maoni

  1. Sadio Mane https://al-nassr.sadio-mane-ar.com the Senegalese footballer best known for his performances at clubs such as Southampton and Liverpool, has become a prominent figure in Al Nassr.

  2. Monica Bellucci https://dracula.monica-bellucci-ar.com one of the most famous Italian actresses of our time, has a distinguished artistic career spanning many decades. Her talent, charisma, and stunning beauty made her an icon of world cinema.

  3. Автомобили Hongqi https://hongqi-krasnoyarsk.ru в наличии – официальный дилер Hongqi Красноярск

  4. After some difficult years in the late 2010s, Manchester United https://england.manchester-united-ar.com returned to greatness in English football by 2024.

  5. Michael Jordan https://chicago-bulls.michael-jordan-ar.com is one of the greatest basketball players of all time, whose career with the Chicago Bulls is legendary.

  6. The golf https://arabic.golfclub-ar.com industry in the Arab world is growing rapidly, attracting players from all over the world.

  7. In recent years, the leading positions in the Spanish https://spanish-championship.laliga-ar.com championship have been firmly occupied by two major giants – Barcelona and Real Madrid.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *