WAZIRI DKT.NDUMBARO AZITAKA NCHI ZA AFRIKA KUWA NA KAULI MOJA KUHUSIANA NA BIASHARA YA UWINDAJI WA KITALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amezitaka nchi za Afrika kuwa na kauli moja kuhusu taratibu na bei  za wanyamapori  katika biashara uwindaji wa kiutalii

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao  ana  kwa ana na baadhi ya  mawaziri wa Utalii wa nchi za Afrika katika Mkutano wa 64 wa  Kimataifa wa Utalii uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii Duniani  (INWTO) unaofanyika kwa muda wa siku nne nchini Cape Verde.

Ad

Amesema bei za wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa pamoja na vitalu vya uwindaji wa Wanyamapori zimekuwa zikitofautiana sana kati ya nchi na hali hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa shughuli uhifadhi barani Afrika.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (wa pili kuli) akiwa kwenye picha ya pamoja na na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe mara baada ya kikao cha kujadili uwindaji wa kitalii pembeni mwa Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.Kulia ni Balozi wa Paris Ufaransa Mhe.Samweli Shekindo pamoja Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ya Zimbabwe Dnomal dinamo

Akizungumza katika vikao hivyo vya ana kwa ana na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe.Mhe.Ngobhithize Ndlovu  amezitaka nchi hizo kuwa kitu kimoja katika kuamua na kupanga bei za uwindaji wa Kitalii.

Amesema kutokana na kutofautiana kwa bei na baadhi  ya kanuni na taratibu hizo  Wawindaji wa kiitalii wamekuwa wakitumia mwanya huo  kuzikandamiza nchi za Kiafrika kwa kupanga bei wanazotaka wao huku wakidai kuwa bei hizo cha chini zimekuwa katika nchi nyingine pia.

Amesema Wawindaji hao wamekuwa wakipanga  bei za uwindaji wa kiutalii na sio nchi husika huku wakidai kuwa kama bei hiyo haitawezekana basi watakwenda katika nchi nyingine ambayo utalii wake uwindaji ni bei ya chini zaidi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na Waziri wa Utalii wa Nigeria, Alhaji Mohammed katika mara baada ya Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla ambapo wamekubaliana kushirikiana katika kutangza vivutio vya utalii kwa pamoja kama Bara la Afrika.

“Utofauti wetu huu umekuwa ukitukandamiza kama nchi kwani tulitakiwa sisi ndo tupange bei lakini kutokana na kutokuwa na umoja bei za wanyama  zimekuwa zimekuwa zikiamuliwa na wao  hili lazima tulikatae kwa kuungana kwa pamoja ” alisisitiza Dkt.Ndumbaro

Kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro amezitaka nchi zote zinazoendesha utalii wa uwindaji zifanye mkutano kwa nji ya mtandao ili kujadili mustakabali wa biashara hiyo na kisha  zitoke na kauli moja ili kuwathibiti wawindaji wa kitalii kwa ajili ya maslahi mapana ya uhifadhi barani Afrika.Amezitaja baadhi ya nchi wanachama wa SADC zinazofanya vizuri katika uwindaji wa kitalii kuwa ni Botswana, Zimbabwe pamoja, Zambia na Afrika ya Kusini 
Katika hatua nyingine , Dkt.Ndumbaro ametoa ahadi kwa  nchi ya Zimbabwe  kama itakuwa  tayari ipewe mafunzo ya kuendesha biashara ya uwindaji wa kiutalii kwa mfumo wa kidigitali ambao utasaidia kuongeza mapato maradufu

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na Waziri wa Utalii wa Kenya , Mhe. Najib Balala katika mara baada ya Mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla ambapo wamekubaliana kushirikiana katika kutangza vivutio vya utalii kwa pamoja kama Bara la Afrika.

Amesema tangu kuanzisha kwa mfumo huo nchini Tanzania umeleta manufaa makubwa kwa nchi  ambapo Wawindaji wa kitalii ili kuweza kupata vitalu vya uwindaji wamekuwa wakilazika kushiriki katika mnada wa kimtandao.

Naye, Waziri waUtalii wa ZimbabweMhe.Ngobhitithize Ndlovu amesema nchi za kiafrika lazima ziungane katika suala hilo kwani katika nchi ya Zimbabwe Wawindaji hao pia wamekuwa wakipanga bei huku wakidai kama hiyo bei haitawezekana watakwenda Tanzania ambako bei vitalu vya uwindaji ipo chini zaidi

Amesisitiza kuwa shughuli za uhifadhi zimekuwa aghali sana huku biashara hiyo ya uwindaji wa kiutalii ukibaki pale pale kutokana na kutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine

Naye, Kamishna Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi amesema umoja huo wa nchi za Kiafrika katika biashara ya vitalu vya uwindaji italiingizia taifa fedha nyingi za kigeni sio kwa Tanzania pekee bali kwa Afrika nzima

” Biashara hiyo imekuwa na ushindani baina yetu bila kujuana kufuatia kila nchi kupanga bei zake kulingana na matakwa ya wadau hao huku shughuli za uhifadhi zikiwa juu zaidi” amesisitiza Kamishna Mabula.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *