ZIARA YA KATIBU MKUU DKT. JOHN JINGU GEREZA KUU LA ISANGA DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kazi nzuri ya kuhakikisha mahabusu na wafungwa magerezani wanapata usimamizi mzuri na kutatuliwa changamoto zao.

Dkt. Jingu ameyasema hayo akiwa katika Gereza Kuu la Isanga Jijini Dodoma ikiwa ni ziara yake katika Magereza mbalimbali nchini yenye lengo la kusikiliza wafungwa na mahabusu hususani wenye changamoto zinazohusu masuala ya Ustawi wa Jamii.

Ad
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu la Isanga, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Fumbuka Ikobela mara baada ya kuwasili katika gereza hilo jijini Dodoma yenye lengo la kusikiliza wafungwa na mahabusu hususani wenye changamoto hasa zinazohusu masuala ya Ustawi wa Jamii.

Aidha Dkt. Jingu ameitaka jamii kuwatambua wafungwa na mahabusu kuwa ni sehemu ya jamii kwa kuwatembelea na kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali yatakayosaidia kutatua changamoto zao.

“Wafungwa hawa wametokana na jamii inayotuzunguka hivyo hatuna budi kuwasikiliza na sisi tumesikia changamoto zao tunakwenda kuzifanyia kazi na nyingine zilizo nje ya uwezo wetu tutashirikiana na wenzetu Serikalini tuone namna ya kuzitatua”. alisema Dkt. Jingu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza Kuu la Isanga, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Fumbuka Ikobela, amesema ziara wa Katibu Mkuu Dkt. Jingu ni faraja kwao kwani ni hatua muhimu ya kufikisha changamoto zinazowakabili mahabusu na wafungwa na kufanyiwa kazi.

“Katibu Mkuu amesikiliza changamoto mbalimbali zilizopo gerezani na ninaamini zile zilizo ndani ya uwezo wake zitafanyiwa kazi kwa wakati na zilizo zaidi ya uwezo wake ataziwasilisha kwa wahusika, nimuombe aendelee kutembelea magerezani kwani nayo ni sehemu ya Jamii” amesema Mkuu huyo wa Gereza.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Angola Mhe. Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Luanda nchini Angola tarehe 08 Aprili, 2025

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *