WAZIRI JAFO AFANYA ZIARA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MUONGOZO WA USAFISHAJI MITO JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo akiongea na Kikosi kazi cha usimamiaji na utekelezaji wa muongozo wa usafishaji mchanga kwenye Ofisi za NEMC Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo amefanya ziara kwenye Mto Mbezi na Msimbazi kukagua namna utekelezaji wa muongozo wa usafishaji mito Mkoa wa Dar es Salaam uliotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na kubaini kuwa unafuatwa.

Akiongea kwenye ziara hiyo Waziri Jafo amekipongeza kikosi kazi kinachosimamia muongozo huo ambacho kinajumuisha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Halmashauri zote za Wilaya  za Mkoa wa Dar es Salaam.

Ad

“Nakipongeza kikosi kazi kwa kazi kubwa ya kulinda mazingira yetu, kinahakikisha  masharti yaliyotolewa kwenye vibali vya kusafisha mito yanafuatwa na mpaka sasa ni takribani kilometa 47 zimeshasafishwa” amesema Mhe. Jafo

Mhe. Jafo ameongeza kuwa ukifuatwa utaratibu mzuri wa kusafisha mito kama muongozo unavyotaka itasaidia kuepuka uharibifu wa kingo za mito jambo ambalo linasababisha kuhama kwa mtiririko wa  maji ya mto katika asili yake na kuleta mafuriko.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya usimamiaji muongozo wa usafishaji mito Jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine Mhe. Jafo amepiga marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga bila kufuata utaratibu uliowekwa wa kusafisha mito.

” Hatua kali za Kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika anachimba mchanga bila  kibali cha bonde au mamlaka husika”.

Aidha Mhe. Jafo amewataka Wakandarasi wote wanaofanya shughuli za usafishaji mito wafanye kazi kwa weledi na wazingatie masharti yaliyowekwa na Serikali.

Naye Kaimu Mkurugenzi (Kurugenzi inayosimamia utekelezaji na usimamiaji wa Sheria ya mazingira) kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi (NEMC) Mhandisi Redemta Samwel amesema Sheria ya Mazingira ni suala mtambuka, linaanzia kwenye ngazi ya Taifa mpaka kwenye familia kwahiyo kila mmoja anawajibika katika utunzaji wa mazingira.  Ameongeza kuwa uchimbaji wa mchanga holela kwenye mito ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli zozote za kudumu kwenye vyanzo vya maji ndani ya mita 60.

“Sheria ya Mazingira inazuia kufanya shughuli za kudumu ndani ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji, hivyo kuchimba mchanga bila kuwa na utaratibu na kibali maalumu ni kuvunja Sheria ya Mazingira”.

Naye Dkt. Elizabeth Mshote Kaimu Mwenyekiti wa kikosi kazi cha usimamizi wa usafishaji mito amesema  shughuli ya usafishaji mito unaenda sambamba na utunzaji wa kingo, kuondoa taka ngumu na tope ndani ya mito na jambo hili linaendea kufanywa vizuri na Wakandarasi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *