HESLB NA TASAF KUWEZESHA WANAFUNZI WA KAYA MASKINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo ameitaka Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kuendeleza mashirikiano yaliyopo ili kuhakikisha watanzania wahitaji wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu wanawezeshwa.

Akizungumza katika Hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Sebastian Inoshi, wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) baina ya taasisi hizo leo Jijini Dodoma, Dkt. Akwilapo alisema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za Serikali kushirikiana katika kuwafikia wananchi na kutoa huduma.

Ad
2. Mkurugenzi Mtendaji Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga wakibadilishana Hati ya Makubaliano Baina ya Taasisi hizo wakati wa Hafla iliyofanyika leo Jumatano Septemba 15, 2021 Jijini Dodoma.

Dkt. Akwilapo aliongeza kuwa ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa Watanzania wahitaji wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu wanapata mikopo ya elimu ya juu na kutimiza ndoto zao, hivyo upo umuhimu mkubwa wa TASAF na Bodi ya Mikopo kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kama inavyotarajiwa.

“Katika hili naomba niwape takwimu, mwaka 2019/2020, Serikali ilitoa TZS 450Bilioni zilizowanufaisha jumla ya wanafunzi 132,392, Bajeti hii imeongezeka hadi kufikia TZS 570 Bilioni mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 ambazo zitawanufaisha jumla ya wanafunzi 160,000alisema Dkt. Akwilapo.

3. Mkurugenzi Mtendaji Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga wakibadilishana Hati ya Makubaliano Baina ya Taasisi hizo wakati wa Hafla iliyofanyika leo Jumatano Septemba 15, 2021 Jijini Dodoma.

Aidha Dkt. Akwilapo aliitaka Bodi ya Mikopo na TASAF ziongeze kasi ya kuunganishwa kwa mifumo ya TEHAMA ili kuwezesha utambuzi wa haraka na uhakika wa wanafunzi wanaotoka katika kaya masikini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaopata udahili katika taasisi za elimu ya juu nchini na ambao wapo katika mpango wa TASAF wanapata mikopo ya elimu ya juu na kutimiza ndoto zao.

 “Makubaliano haya yatasaidia kuongeza ufanisi katika kubadilishana taarifa, hivyo na HESLB imejipanga kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu, Wanafunzi wahitaji wahakikishe wanatimiza wajibu wao kwa kuomba mkopo kwa usahihi” alisema Badru.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Hafla ya Utiaji Saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakati wa Hafla iliyofanyika leo Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Ikulu), Moses Kusiluka.

Naye Mkurugenz Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga alisema taasisi hiyo itahakikisha inasimamia kwa umakini mkubwa malengo ya mashirikiano hayo ili kuhakikisha wanafunzi wahitaji wanaotoka katika kaya maskini wanapata mikopo YA elimu ya juu kutoka HESLB.

Mashirikiano haya yanaiwezesha HESLB kama taasisi ya mikopo ya wanafunzi kupanga mikopo kwa wanafunzi wahitaji kutoka katika Mpango wetu, tumejipanga kuhakikisha kuwa mifumo yetu kuwatambua kwa haraka wanafunzi wote ambao wanakidhi vigezo vya HESLB katika kupangiwa mikopo ya elimu ya juu” alisema Mwamanga. 

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *