WAMACHINGA – TUPO TAYARI KUPANGWA KWENYE MAENEO RASMI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo September 16 amefanya kikao Cha pamoja na uongozi wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam kuhusu njia Bora ya Kuwapanga Machinga Jijini humo.

Katika kikao hicho Uongozi wa Machinga umepongeza hatua ya RC Makalla kutumia njia ya shirikishi Jambo lililotoa fursa kwa Machinga kuwa huru kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali yenye mrengo wa kufanikisha maelekezo ya Serikali.

Ad

Akizungumza Katika kikao hicho RC Makalla amefurahi kuona kikao hicho kimemalizika kwa Mafanikio makubwa ambapo ameahidi kushughulikia mapendekezo yote yaliyotolewa kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya.

Aidha RC Makalla amesema miongoni mwa maeneo atakayoanza kuyafanyia kazi ni pamoja na kuwapanga Machinga waliojenga Vibanda juu ya Mitaro na mifereji, Wanaofanya biashara Kwenye njia za watembea kwa miguu, wanaofanya biashara mbele ya Maduka, wanaofanya biashara Kwenye hifadhi ya Barabara na wanaofanya biashara mbele ya Taasisi za Umma zikiwemo shule.

Pamoja na hayo RC Makalla ametoa Fursa kwa Viongozi wa Machinga kupendekeza maeneo ya Wazi wanayoona yanafaa kwa biashara ili wapatiwe na ameahidi kuweka mazingira Bora ya biashara ikiwemo kufikisha huduma ya Usafiri.

Hata hivyo RC Makalla amesema Serikali itaendelea kutoa elimu ya kutosha Wafanyabiashara kwakuwa lengo la Serikali ni kuona biashara zinafanyika na watu wanapata kipato.

Kwa upande wao Viongozi wa Machinga akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Machinga Bwana Steven Lusinde amemshukuru RC Makalla kwa uamuzi wa kukutana nao na kuwasikiliza Jambo lililowezesha kila upande kutoa maoni na mapendekezo ya namna Bora ya kufanikisha Mpango huo na Wana Imani kwa Mpango wa kuwapanga Machinga Dar es salaam utakuwa na mafanikio makubwa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *