WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA UONGOZI WA EQUINOR NA SHELL

Na Dorina G. Makaya na Janeth Mesomapya – Dar-es-Salaam

Waziri wa Nishati January Yusuf Makamba, leo tarehe 24 Septemba, 2021 amekutana na uongozi wa kampuni za Equinor na Shell kwa lengo la kufahamiana na kufanya mazungumzo mafupi kuhusu kuanza kwa majadiliano ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) wa Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG).

Katika kikao hicho Waziri Makamba, ameuhakikishia uongozi wa kampuni za Equinor na Shell kuwa, Serikali ya Tanzania iko tayari kuanza majadiliano ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) ambayo yanatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Octoba, 2021.

Aidha, wadau hao wameihakikishia Serikali kwamba wako tayari kwa ajili ya kuanza majadiliano na kuwa timu yao itakayoongoza majadiliano hayo tayari iko jijini Dar-es-Salaam.

Kwa upande wa Wizara ya Nishati, baadhi ya viongozi waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, Kamishna wa Petroli na Gesi Adam Zuberi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt. James Mataragio na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mha. Charles Sangweni.

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.