WAZIRI MKENDA AWATAKA WADAU WA NDIZI KUCHANGAMKIA FURSA

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa wadau wa zao la ndizi Kanda ya Kaskazini uliofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Septemba 25, 2021.

Waziri wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda, amewataka wadau wa zao la ndizi nchini ikiwemo wawekezaji kuchangamkia frusa ya kuzalisha kwa wingi zao hilo ambalo kwa sasa limewekewa mkakati wa kuwa zao kubwa la kibiashara.

Profesa Mkenda ameyasema hayo Leo tarehe 25 Septemba 2021 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akifungua mkutano wa wadau wa zao hilo Kanda ya kaskazini ambapo amesema pamoja na wizara hiyo kuthamini na kuyapa kipaumbele mazao mengini lakini pia ndizi ni zao muhimu kibiashara.

Ad
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa wadau wa zao la ndizi Kanda ya Kaskazini uliofanyika Moshi, Septemba 25, 2021.

Amesema serikali ipo tayari kuwaunga mkono wadau wote ikiwemo wa uwekezaji  na wakulima wakubwa wa zao hilo kutokana na kwamba wizara ya Kilimo imelipa umuhimu mkubwa kwa lengo la kuwa zao la kibiashara.

Amesema kuwa, katika nchi nyingine zao hilo limekuwa likizalishwa kwa wingi ambapo kwa mwaka huzalishwa kwa Tani elfu 60 hadi 70 na kuuzwa maeneo mbalimbali Duniani na kuzinufaisha nchi hizo kiuchumi na kwamba wawekezaji wanapaswa kuona fursa hiyo.

“Zao la ndizi ni muhimu kama zao la chakula na Kama matunda lakini kwa namna tunavyo shughulika na kilimo hichi ni tofauti na nchi nyingine ambapo hulilima kama zao la biashara hivyo naombeni wadau mchangamkie frusa hii kwani serikali ina mkakati wa kuhakikisha zao hili linakuwa la biashara” Amesema Profesa Mkenda

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa wadau wa zao la ndizi Kanda ya Kaskazini uliofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Septemba 25, 2021.

Aidha, amesema katika kuhakikisha zao hilo linazalishwa kwa tija, serikali itahakikisha inaongeza na kuboresha  huduma za ugani ikiwa ni pamoja upatikanaji wa mbegu bora kwa kushirikiana na wadau.

“Serikali ipo na tutahakikisha tunashirikiana na wadau wote kwa kufanya kazi nanyi bega kwa bega na naomba tushikamane wote tuendeleze zao hili kama ilivyo kwa mazao mengine” Amesema Mkenda

Sehemu ya Wabunge wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa wadau wa zao la ndizi Kanda ya Kaskazini uliofanyika Moshi, Septemba 25, 20221.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, ameziagiza Halmashauri za wilaya nchini kujenga vituo vya ukusanyaji wa zao hilo kwa kuwawezesha vijana kwa kuwakopesha asilimia 10 ya mapato inayotengwa.

Amesema kuwa (TAMISEMI) inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau wake katika kuhakikisha watanzania wananufaika na zao hilo pamoja na mazao mengine na kwamba serikali wamekuja na mpango wa kuhakikisha wakulima wa ndizi wanaongeza thamani ya ndizi.

Naye Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya mbogamboga, Maua na matunda(TAHA), Dkt Jackline Mkindi amesema kuwa lengo la kuwakutanisha wadau hao ni kwa ajili ya kuaandaa mkakati wa pamoja wa kufufua zao la ndizi kitaifa na kimataifa ili kukabiliana na changamoto ya masoko ya zao hilo na kuongeza mnyororo wa thamani.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *