RAIS SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA WACHUNGAJI NA MAASKOFU NA MMADHIMISHO YA MIAKA 50 YA ANGLKANA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kongamano la Wachungaji na Maaskofu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Maadhimisho ya Miaka 50 Kanisa hilo katika Viwanja vya Chuo Kikuu ST. John’s Jijji Dodoma leo Sept 28,2021. Caption.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali imedhamiria kwa dhati kuwainua Wanawake kijamii, kiuchumi, kisiasa pamoja na kupambana na ukatili dhidi yao.

Rais Samia amesema hayo leo tarehe 28 Septemba, 2021 wakati akihutubia kwenye Maadhimisho ya Miaka 50 na Kongamano la Wachungaji na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania katika Chuo Kikuu cha St. John’s Jijini, Dodoma.

Ad

Rais Samia amesema Serikali inafanya hivyo sio kwasababu kuwa yeye ni Rais Mwanamke, bali kwa kuwa mwanamke ana haki sawa kama mwanaume isipokuwa kinachowatofautisha ni makuzi na imani zao.

Aidha, Rais Samia ametolea mfano wa Wanawake hapa nchini kuwa wapo zaidi ya asilimia 50 hivyo kama wakiachwa nyuma maendeleo hayawezi kupatikana kwa urahisi.

Pia, Rais Samia ameeleza kuwa hapendi kuona Mwanamke akiwekwa kama mtu wa  daraja la chini na kubainisha kuwa  dhamira yake kwa sasa ni kuwanyanyua wanawake na ameliomba Kanisa hilo kumuunga mkono katika jitihada hizo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kongamano la Wachungaji na Maaskofu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Maadhimisho ya Miaka 50 Kanisa hilo katika Viwanja vya Chuo Kikuu ST. John’s Jijji Dodoma leo Sept 28,2021. Caption.

Vilevile, Rais Samia amelipongeza na kulishukuru Kanisa hilo la Anglikana Tanzania kwa kazi kubwa ya kuhubiri Injili na kuwalea wananchi kiroho na kimaadili hali iliyopelekea kuchangia kwa kiasi kikubwa kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Rais Samia amesema mafundisho yanayotolewa na Kanisa hilo kwa waumini wao pamoja na yale yanayotolewa na dini na madhehebu mengine ndio yanayosaidia nchi kuwa na amani, umoja na mshikamano.

Aidha, Rais Samia amesema mbali na Kanisa hilo kuwalea wananchi kiroho pia lina mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii ambapo mpaka sasa Kanisa Anglikana lina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 40, vyuo vya afya 7 na taasisi za elimu 63, kikiwemo Chuo Kikuu cha St. John’s Jijini Dodoma.

Mhe. Rais Samia ameeleza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika utoaji huduma hizo za jamii ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikopo ya elimu ya juu wanafunzi wa Vyuo Vikuu vinavyomilikiwa na Kanisa hilo.

Vilevile, Rais amesema Serikali itaendelea kutoa vifaa tiba, vitendanishi, kuajiri na kulipa mishahara ya watumishi wa afya kwenye vituo vya afya na Hospitali ilizoingia makubaliano ya kuendesha kwa ushirikiano.

Rais Samia amewaomba viongozi wa dini nchini kuzungumzia suala la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwakani 2022 na bila kusahau kujikinga na janga la UVIKO 19 kila wanapokutana na waumini wao.

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Nani aliyeunda Jumuiya ya Madola na kwa nini?”

Malkia Elizabeth II pamoja na mawaziri wake wakuu wa Jumuiya ya Madola mwaka 1962. Picha: …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.