RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA IKULU CHWAMWINO

Rais Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 28 Septemba, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Rais Samia amemueleza Dkt. Ghanem vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita ambavyo ni kuboresha huduma za jamii ikiwemo elimu na afya pamoja na ujenzi wa miradi ya kimkakati.

Ad

Aidha, Rais Samia amemueleza Dkt. Ghanem kuwa kwa sasa Serikali inapitia sera zake za kodi kwa majadiliano na wadau ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika kuimarisha sekta binafsi ili iweze kushindana na kuchangia ajira nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo Sept 28,2021.

Rais Samia pia amezungumzia jitihada zinazofanywa na Serikali kuweka taarifa na kuongeza ufanisi katika makusanyo kupitia matumizi ya TEHAMA.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Ghanem amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kushirikiana na Benki ya Dunia katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo Sept 28,2021.

Aidha, Dkt. Ghanem ameeleza dhamira ya Benki ya Dunia ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwajengea uwezo wanawake kiuchumi kuanzia wanapozaliwa, kimasomo na katika afya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo Sept 28,2021.

Pia, Dkt. Ghanem amesema Benki hiyo ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika ununuzi, usafirishaji na utoaji elimu ya UVIKO 19 kwa jamii ili kutoa muamko kwa wananchi kujitokeza kupata chanjo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Nani aliyeunda Jumuiya ya Madola na kwa nini?”

Malkia Elizabeth II pamoja na mawaziri wake wakuu wa Jumuiya ya Madola mwaka 1962. Picha: …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *