WAZIRI MCHENGERWA AELEKEZA KUWASHUSHA VYEO MAAFISA UTUMISHI WALIOSHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA KUWAPANDISHA VYEO WATUMISHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaelekeza watendaji wa ofisi yake kufanya ufuatiliaji ili kuwashusha vyeo Maafisa Utumishi katika Taasisi za Umma walioshindwa kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hasssan la kuwapandisha vyeo watumishi wenye sifa za kupanda madaraja.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Ad
Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Mhe. Mchengerwa amesema, Afisa Utumishi yeyote aliyezembea na kusababisha Watumishi wa Umma kutopandishwa madaraja achukuliwe hatua kwa kushushwa cheo na kuhamishwa kituo cha kazi ili iwe ni fundisho kwa wengine wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo.

“Fanyeni upembuzi na kuwaondoa Maafisa Utumishi wote waliobainika kutotekeleza wajibu wa kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa stahiki, kwani nimekuwa nikipokea malalamiko toka kwa watumishi wa taasisi mbalimbali,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Ameongeza kuwa, ofisi yake ilifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha taarifa za kiutumishi zilizotumwa na waajiri zinafanyiwa kazi kwa lengo la kuwapandisha vyeo watumishi husika, hivyo amewapongeza watendaji wa ofisi yake kwa kutekeleza vema wajibu wao.

Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda akitoa neno la utangulizi kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa, Mhe. Rais anawajali sana Watumishi wa Umma na ndio maana alitoa agizo la kuwapandisha vyeo katika kipindi ambacho mijadala ya bajeti Bungeni ilikuwa ikiendelea jambo ambalo katika hali ya kawaida isingekuwa rahisi kutekelezeka.

“Mhe. Rais anatambua kuwa nguzo ya Serikali kiutendaji ni Watumishi wa Umma hivyo haiwezi kufanya vizuri iwapo haitowajali watumishi wake na ndio maana aliagiza wapandishwe madaraja,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika amemshukuru Mhe. Waziri kwa kukubali wito wa kukutana na Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali na kumuahidi kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali mara baada ya kufungua kikao kazi cha watendaji wakuu hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Dkt. Shindika amemhakikishia Mhe. Mchengerwa kuwa Watendaji Wakuu hao wa Wakala za Serikali watahakikisha wanahimiza uwajibikaji kwa Maafisa Utumishi wao ili waendane na kasi ya kiutendaji ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amehimiza uwajibikaji kwa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali ili waweze kuendana na Kaulimbiu ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya KAZI IENDELEE.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

158 Maoni

  1. Здравствуйте!
    Приобрести диплом о высшем образовании.
    yobasket.es/es/perfil-usuario/pluginclass/cbblogs.html?action=blogs&func=show&id=121

  2. [u][b] Привет![/b][/u]
    [b]Купить диплом университета.[/b]
    [url=http://fatshipresident.net/read-blog/217/]fatshipresident.net/read-blog/217[/url]

  3. [u][b] Добрый день![/b][/u]
    [b]Полезные советы по безопасной покупке диплома о высшем образовании [/b]
    [url=http://kryza.network/create-blog/]kryza.network/create-blog[/url]
    Рады оказать помощь!

  4. [u][b] Привет, друзья![/b][/u]
    [b]Мы предлагаем дипломы[/b] любых профессий по выгодным тарифам.
    [url=http://bence.net/read-blog/59_proverennyj-onlajn-magazin-s-ogromnym-assortimentom-diplomov.html?mode=night/]bence.net/read-blog/59_proverennyj-onlajn-magazin-s-ogromnym-assortimentom-diplomov.html?mode=night[/url]

  5. Добрый день!
    Мы готовы предложить документы ВУЗов, которые расположены в любом регионе Российской Федерации. Можно заказать диплом от любого заведения, за любой год, включая документы старого образца СССР. Дипломы и аттестаты печатаются на “правильной” бумаге высшего качества. Это дает возможности делать настоящие дипломы, которые не отличить от оригиналов. Они заверяются необходимыми печатями и подписями.
    islider.ru/read-blog/828

  6. Здравствуйте!
    Пошаговая инструкция по безопасной покупке диплома о высшем образовании
    msfo-soft.ru/msfo/forum/messages/forum28/topic9959/message278494/?result=new#message278494
    Будем рады вам помочь!.

  7. It has been calculated that ten million people could die from antibiotic resistant bacterial infections each year by 2050 39 priligy ebay However, women consistently report worse health status and greater morbidity symptoms than men do

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *