RAIS SAMIA AWATAKA WADAU WA MFUMO WA UTOAJI HAKI NCHINI KUZINGATIA SHERIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 06 Oktoba, 2021 amezindua Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma kwa niaba ya vituo vingine 5 katika mikoa mitano hapa nchini vilivyogharimu shilingi bilioni 51.53.

Vituo vingine 5 vimejengwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam vituo viwili (Temeke na Kinondoni), ambapo kituo cha Temeke kitakuwa mahsusi kushughulikia mashauri ya kifamilia, mirathi, ndoa, talaka, malezi na matunzo.

Ad

Rais Samia amesema ujenzi wa kituo cha Temeke Jijini Dar es Salaam kitasaidia kupunguza mlundikano wa kesi za namna hiyo, lakini pia kitatumika kama Chuo cha kutoa mafunzo ya namna ya kushughulikia migogoro ya mirathi, ndoa, malezi na matunzo nchi nzima.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu sehemu ya uendeshaji Haki mara baada ya kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu sehemu ya uendeshaji Haki mara baada ya kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa Dodoma Antoni Mtaka.

Aidha, Rais Samia ameipongeza Mahakama kwa kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Vituo Jumuishi sita vya utoaji Haki (Intergrated Justice Centres) ambao ni  muhimu katika kusimamia utoaji haki nchini, kudumisha amani hususan kupitia usuluhishi wa migogoro mbalimbali inayotokea kwenye jamii pamoja na kukuza uchumi.

Amesema katika vituo hivyo kutakuwa na mahakama za ngazi zote kuanzia Mahakama ya Mwanzo, Wilaya, Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu na pia eneo kwa ajili ya Mahakama ya Rufani.

Rais Samia amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Mahakama kukutana na viongozi wa Wizara ya Mawasiliano na Wizara ya Fedha kushughulikia changamoto ya gharama ya Bandwidth ili  Mahakama iweze kutekeleza majukumu yake kimalifu kupitia mfumo wa TEHAMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuzindua Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki vya Mahakama ya Tanzania katika hafla iliyofanyika katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021.
Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Tanzania ambacho kimezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021.
Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Tanzania ambacho kimezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021.

Pia, Rais Samia ameagiza Mahakama ihakikishe kuwa kwenye mpango mkakati wa miaka mitano ijayo ya maboresho ya Huduma za Utoaji Haki, mikoa 9 isiyokuwa na Mahakama Kuu ambayo ni Njombe, Geita, Singida, Manyara, Pwani, Katavi, Songwe, Lindi na Simiyu ipewe kipaumbele, zikiwemo kata na wilaya ambazo hazina Mahakama.

Vilevile, Rais Samia amewataka wadau wote wa mfumo wa utoaji haki nchini kuzingatia sheria, taratibu na kuongozwa na nafsi zao katika kufanya maamuzi ili kuwe na mafanikio yanayotarajiwa.

Rais Samia ameitaka Mahakama kushughulikia suala la ucheleweshwaji wa kesi na kumuomba Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi kuongeza usimamizi wa ubora wa maamuzi kwenye Mahakama za Mwanzo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *