RAIS SAMIA KUZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI MLANDIZI – MBOGA MACHI 22

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

Mradi mkubwa wa maji Mlandizi-Mboga (Chalinze) mkoani Pwani uliogharimu Bilioni 18, unatarajiwa kuzinduliwa Machi 22 mwaka huu ,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan.

Ad

Mradi huo unatajwa kwenda kuondoa kero kubwa ya maji waliyokuwa wakiipata wananchi Chalinze na maeneo jirani .

Akitoa taarifa ya ujio huo wa Rais, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge alisema ni bahati iliyoje kwa Wana Pwani, kuona Rais imempendeza kufanya ziara fupi na uzinduzi wa mradi huo eneo la Msoga ikiwa ni sehemu ya kilele Cha wiki ya maji .

“Mradi huu unaanzia Mlandizi,umejengwa vituo vidogo vya maji Chamakweza na Mboga Lengo maji yafike kwenye maeneo yenye shida ya maji “

“Hii ni wiki ya maji na kilele ni Machi 22 ambapo Rais itakuwa sehemu ya maadhimisho,Imani yetu shughuli itaanza mapema hivyo wananchi waje kuunga mkono Jambo hili “alieleza Kunenge.

Licha ya kuzindua mradi wa maji pia atazungumza na wananchi kiwanja cha polisi Chalinze.

Hata hivyo, Kamisaa huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kunenge aliwataka wanaCCM kujitokeza katika ziara hiyo fupi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa.

“Maeneo yatakayohudumiwa na mradi huo ni pamoja na Ruvu darajani, Vigwaza, Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi.
Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa .

Vilevile, Mkuu huyo wa mkoa ,alisema mkoa unaendelea kuisimamia miradi mbalimbali na kutatua kero za wananchi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *