DKT. YONAZI AMELIKUMBUSHA JESHI LA POLISI WAJIBU WA KUJIFUNZA NA KUTOA ELIMU YA USALAMA MTANDAO

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) CP Camilius Wambura akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amelikumbusha Jeshi la Polisi Tanzania kuwa linalo wajibu wa kujifunza na kuwaelimisha wengine kuhusu makosa ya mtandao, namna ya kujilinda na kuchukua tahadhari dhidi ya makosa ya mtandao

Dkt. Yonazi ametoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya usalama mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar yanayofanyika kwa siku tano jijini Dodoma kuanzia tarehe 21 Machi hadi tarehe 25 Machi, mwaka 2022

Ad

Amesema kuwa, Jeshi la Polisi linalo wajibu wa kujifunza kila siku, kwa kuwa wao pia ni washirika katika ulimwengu wa mtandao kupitia matumizi ya simu janja lakini pia Wimbo wa Jeshi la Polisi unasema wazi kuwa wana jukumu la kulinda usalama na haki za wananchi ambapo utekelezaji wa jukumu hilo unafanyika katika ulimwengu mpya wa kidijitali

Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, (DCP) Ally Lugendo akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.

“Dunia inabadilika kuna uhalifu mwingi unaofanyika kwa njia ya mtandao na watu wa makundi yote kwa kukusudia au bila kukusudia, hivyo watendaji mnapopatiwa elimu mna wajibu wa kuelimisha wengine kupitia nafasi za utendaji mlizo nazo sasa”, Amezungumza Dkt. Yonazi

Ameongeza kuwa, “Ukimchapa mtoto lazima umfahamishe kwanini umemchapa na kosa ni lipi, vivyo hivyo kwenye makosa ya mtandao, kabla ya kuyashughulikia ni vema wananchi wapatiwe elimu na kufahamu makosa ya mtandao ni yapi”.

Dkt. Yonazi ameyazungumzia mafunzo hayo kuwa yanatoa taswira nzima na uelekeo wa nchi katika kushughulikia masuala ya usalama mtandao ili kufikia malengo yanayotarajiwa huku wajibu wa Wizara hiyo ni kuhakikisha mafunzo hayo ni endelevu na usalama katika mtandao unasimamiwa vizuri

Mkaribu Mwandamizi wa Polisi, (SSP) Joshua Mwangasa akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.

Akizungumza na hadhira hiyo Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini (DCI) CP Camilius Wambura ameishukuru Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuwezesha mafunzo hayo kwa kuwa yatawasaidia watendaji wa Jeshi la Polisi Tanzania kuongeza ujuzi utakaowafungua zaidi na kupanua wigo wa kupambana na uhalifu hasa wa makosa mtandao

“Teknolojia inabadilika kila kukicha hivyo mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji wetu yanahitajika ili kuendana na kasi ya mabadiliko haya kwa watendaji kupitishwa wapi tulipo na wapi tunaelekea katika kukabiliana na uhalifu wa mtandao”. Amezungumza Wambura

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Usalama Mtandao kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, wakisikiliza kwa umakini hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Usalama Mtandao iliyotolewa na Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, (hayupo pichani) yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.

Na Faraja Mpina na Chedaiwe Msuya, WHMTH, DODOMA

Naye Mkaribu Mwandamizi wa Polisi, SSP Joshua Mwangasa ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuwajengea uwezo watendaji wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na hatua zinazoendelea za kuanza ujenzi wa maabara za uchunguzi wa kisayansi zitakazojengwa kikanda katika mikoa sita ya Mbeya, Arusha Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar ambazo zitasaidia kupanua wigo wa uchunguzi wa makosa ya mtandao.

Mafunzo hayo ya usalama mtandao yanatolewa kwa watendaji wapatao 100 wa Jeshi la Polisi Tanzania ikiwa ni muendelezo wa mafunzo yaliyotolewa mwezi Februari mwaka huu kwa watendaji wengine wa Jeshi hilo na sasa ni zamu ya wasimamizi wao ambao ni Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi kama vile TAZARA na Bandari, Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Mikoa na Wakufunzi wa vyuo vya Polisi nchini.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *