KIKAO UIMARISHAJI MPAKA TZ NA KENYA CHAANZA TARIME

Na Munir Shemweta, WANMM TARIME

Kikao cha Kamati ya pamoja ya Wataalamu wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya kimeanza leo tarehe 11 April 2022 wilayani Tarime mkoa wa Mara.

Ad

Kikao hicho cha Kamati ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili kinachotarajiwa kumalizika April 15, 2022 wilayani humo kitapokea mawasilisho ya kazi iliyofanyika na kutoa muongozo juu ya namna bora ya kutekeleza kazi iliyobaki. 

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho wilayani Tarime mkoani Mara tarehe 11 April 2022 kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mangwela alisema uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya Tanzania na Kenya ulenge kuimarisha mahusiano ya nchi hizo pamoja na kujadili changamoto za maeneo ya mipakani.

Mratibu Msaidizi wa Uimarishaji mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Kenya Joseph Ikorongo akiwasilisha taarifa wakati wa kikao cha pamoja cha wataalamu wa mipaka kutoka Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime tarehe 11 April 2022.

“Pamoja na kuimarishwa mipaka kati ya Tanzania na Kenya lakini bado kuna maeneo ambayo baadhi ya wananchi kutoka kila upande wanaingia na kuendesha shughuli zao hivyo mjadili changamoto hizi kwa kina na kuja na maamuzi yatakayoleta tija” alisema Kanali Mangwela.

Timu ya wataalamu wa Tanzania na Kenya imefanikiwa kukamilisha uimarishaji mpaka wa kimataifa wa awamu ya kwanza na kuanza awamu ya pili iliyosimama kutokana na changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Kenya Balozi Joseph Vungo aliwataka wataalamu wanaoshiriki kikao hicho kuhakikisha wanajadili na kuzitolea maamuzi changamoto kwa amani hasa wakizingatia nchi ya Tanzania na Kenya zimekuwa na mahusiano mazuri.

Sehemu ya washiriki kutoka Tanzania

Kwa mujibu wa Balozi Vungo, maamuzi yoyote yatakayoamuliwa katika kikao hicho yalenge kuleta tija na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo.

Zoezi la uimarishaji mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya awamu ya kwanza  limeanzia hifadhi ya Serengeti / Masai Mara kipande cha Kilomita 60 hadi  eneo la Ziwa Natron kilomita 23 na awamu ya pili inaanzia Ziwa Natron hadi Namanga eneo la Kilomita 110.

Ad

Unaweza kuangalia pia

#LIVEDAY2: JUKWAA LA KODI NA UWEKEZAJI 2024

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.