Tofauti ya Sensa ya Mwaka 2022 na Sensa zilizopita:-
Katika sensa ya mwaka 2022 inatarajiwa kuwa na vitu vipya kama vile;
• Kutenga maeneo ya kijiografia ya kuhesabia watu katika ngazi za kitongoji/mtaa na upatikanaji wa taarifa za kitakwimu katika ngazi za kitongoji/mtaa pamoja na kuwa na mipaka ya kudumu katika ngazi hizo;
• Matumizi ya Vishikwambi (tablets) katika hatua zote za utekelezaji wa sensa kwa lengo la kupunguza gharama;
• Nyongeza ya maswali yatakayowezesha upatikanaji wa taarifa zaidi za kitakwimu ikilinganishwa na Sensa ya Mwaka 2012:-
- Taarifa za kidemografia (umri wakati wa ndoa ya kwanza);
- Maswali yanayohusu ulemavu (Kichwa kikubwa, Mgongo wazi, Kifafa/Epilepsy, Mbalanga/storiasis na Usonji/autism);
- Maswali ya uhamaji kulingana na mapendekezo ya IOM (International Organization of Migration);
- Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho NIDA, vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo, Mzanzibari mkazi, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva);
- Maboresho ya maswali ya shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na idadi ya kaya ziliko kwenye sekta isiyo rasmi;
- Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA
• Takwimu za nyumba (orodha, hali ya umiliki na aina ya nyumba)
• Maswali ya kilimo na mifugo