MAFANIKIO YA SEKTA YA UJENZI KATIKA MKOA WA ARUSHA 

 Sekta ya Ujenzi imepata mafanikio makubwa katika Mkoa wa Arusha. Kupitia juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia TANROADS, kumekuwa na maboresho makubwa katika miundombinu ya barabara na madaraja.

Kulingana na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Mha. Reginald R. Massawe, kumekuwa na ongezeko la kilometa 53 za barabara za lami, ambapo mtandao wa barabara za lami umefikia kilometa 478.78 mwaka 2024. Barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na Wasso-Sale, T/Packers-Bypass, na Kijenge-Usariver.

Ad

Mbali na hilo, zaidi ya kilometa 152 za barabara ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi kwa kiwango cha lami. Miradi mingine inayoendelea ni pamoja na Mianzini-Ngaramtoni Juu, Karatu-Kilimapunda, T/Packgers-Losinyai, Mbaunda-Losinyai, Mto wa Mbu-Selela, na Wasso-Loliondo.

Serikali imeanzisha pia mchakato wa ujenzi wa barabara mpya kama vile Arusha-Kibaya-Kongwa na Karatu-Mbulu-Haydom-Sibiti River-Lalago-Maswa. Ujenzi wa barabara ya Ngaresh-Enguik (Monduli Juu) km 11.66 kwa kiwango cha lami uko katika hatua za mwisho za kutangaza zabuni ya mkandarasi.

Miradi ya madaraja pia imekamilika ikiwa ni pamoja na Daraja la Nduruma na Daraja la Kimosonu. Zaidi ya taa 991 zimewekwa katika barabara mbalimbali za Arusha-Namanga, Arusha-Minjingu, Kijenga-Usariver, Makuyuni-Ngorongoro, Arusha Bypass, na T/packers-Losinyai.

Hizi ni hatua muhimu za maendeleo katika Sekta ya Ujenzi ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Mkoa wa Arusha.

#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Awakaribisha Wawekezaji Katika Nishati ya Jotoardhi Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewakaribisha wawekezaji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *