UZINDUZI WA MKAKATI WA TAIFA WA MATUMIZI YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA 2024-2034
Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034″ ni mpango mpana uliowekwa na serikali ya Tanzania kuboresha matumizi ya nishati safi kwa kupikia. Mkakati huu unalenga kufikia asilimia 80 ya Watanzania watumie nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2033. Mkakati unajumuisha usambazaji wa majiko banifu na gesi asilia, pamoja na kuimarisha miundombinu na elimu kuhusu matumizi ya nishati safi.