Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika kuweka msisitizo juu ya muendelezo wa mageuzi katika Mashirika na Taasisi za Umma kwa lengo la kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi katika Taifa letu la Tanzania kwa manufaa ya Taifa na Watanzania wote kwa ujumla.
Rais Samia amesisitiza kuwa Mashirika ya Kiserikali ambayo ina umiliki wa asilimia 100 ya serikali kuna haha watendaji wake kujifunza kutoka Mashirika ambayo Serikali ina hisa ndogo na kuacha kubweteka.
” ..Magawio makubwa tukuyoyapata hapa leo ni kutoka Kampuni ambazo Serikali ina hisa chache; Ina maana kwa sehemu kubwa ni Private Sector na Serikali tuna hisa chache.. Lakini yale ya kwetu.. yale ya Serikali hamkuyaona hapa; Hayapo! Lakini sera ni zile zile!; mazingira ni yale yale!; ila serikali kuna kubweteka! ‘..mimi ni wa serikali, nikikwama serikali ipo itanipa..’ Lakini hawa wenzetu, wana- struggle.., wanahangaika.., wanatumia mbinu zote za biashara waweze kufanyabiashara na waweze kufanya faida halafu ah.. wao wapate na wanahisa wao waweze kupata. Kwahiyo hii ni meseji kwa yale mashirika yetu ambayo ni asilimia mia (100%)..Mashirika ya kiserikali, hili ni la kuangalia.” Rais Samia