Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi wa TANTRADE Bi Latifa Khamis na Mkurugenzi wa Kampuni ya FREMU Ndugu David Mukisa.
Kampuni hiyo inauza bidhaa za vyakula katika soko la Uingereza kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Uganda, Kenya, Nigeria, Ghana na Rwanda. Kufuatia makubaliano yaliyosainiwa leo, bidhaa za wafanyabiashara wa Tanzania zitaweza kuuzwa katika soko la Uingereza. Katika Hafla ya kusaini Makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza kwa kuwa daraja kati ya TANTRADE na Kampuni ya FREMU. Kwa upande wake Mkurugenzi wa FREMU ameeleza kwamba Jukwaa la Kampuni yake litawezesha wafanyabiashara wa Tanzania kuuza bidhaa zao kwa urahisi katika soko la Uingereza. http://fremu.co.uk